Monday, February 26, 2018

Eden Hazard ni bora zaidi ya Messi na CR7,


Kampuni inayokusanya taarifa za takwimu mbali mbali za michezo iitwayo CIES Football Obsevatory imetoka na taarifa mpya kuhusu kiwango cha wachezaji wenye uwezo mkubwa kwa kukokota mipira(dribles).

STAND UNITED NA PRISONS ZATINGA ROBO FAINALI AZAM SPORTS FEDERATION CUP

TIMU za Tanzania Prisons na Stand United zimekamilisha idadi ya timu nane za kucheza hatua Robo Fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi kwenye mechi zao za jana.

WENGER KIBARUA CHAKE CHAINGIA DOSARI

 
KLABU ya Arsenal itaitathmini nafasi ya Arsene Wenger mwishoni mwa msimu — kukiwa na uwezekano wa kuhitimisha miaka 22 ya Mfaransa huyo.

SIMBA YAZIDI KUKWEA KILELENI MWA LIGI VPL

SIMBA SC imezidi kuukimbilia kwa kasi ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Mbao FC ya Mwanza jioni ya jana  Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi alifunga mabao mawili moja kila kwa kipindi kabla ya kuumia na kutolewa wakati mabao mengine yalifungwa na Shiza Kichuya, Erasto Nyoni na Mghana, Nicholaus Gyan.
Ushindi huo unaifanya Simba itimize pointi 45 baada ya kucheza mechi 19, ikiendelea kukaa kileleni mwa Ligi Kuu, ikifuatiwa na mabingwa watetezi, Yanga wenye pointi 37 za mechi 18, wakati Mbao FC inabaki nafasi ya 10 kwa pointi zake 19 za mechi 19.
 li kuanza kupata mabao, benchi la Ufundi la Simba chini ya kocha Mfaransa, Pierre Lechantre anayesaidiwa na Mrundi, Masoud Juma lililazimika kufanya mabadiliko ya mapema kipindi cha kwanza katika safu ya kiungo kwa kumtoa Said Hamisi Ndemla na kumuingiza Muzamil Yassin baada ya nusu saa.
Mabadiliko hayo yalibadilisha kabisa mwelekeo wa mechi, kutoka Mbao FC kutawala hadi Simba SC ambayo wiki ijayo itamenyana na El Masry ya Misri katika Raundi ya Kwanza ya kombe la Shirikisho Afrika kuuteka mchezo.    
Shiza Ramadhani Kichuya akafungua sherehe za mabao za Simba kwa kufunga bao la kwanza dakika ya 38 akimalizia pasi ya mtokea benchi, Muzamil.
Mganda Emmanuel Okwi akaifungia Simba SC bao la pili dakika ya 40 kwa penalti, baada ya yeye mwenyewe kuanguka kwenye boksi wakati anadhibitiwa na beki wa Mbao, David Mwasa.
Refa Erick Onoka kutoka Arusha akawanyima Simba SC penalti sahihi zaidi ya aliyowapa mwanzo baada ya Okwi kuangushwa kwenye boksi na Nahodha wa Mbao FC, Mrundi, Yusuph Ndikumana ambaye leo alicheza chini ya kiwango.
Kipindi cha pili, Mbao FC wanaofundishwa na kocha Mrundi, Etienne Ndayiragijje walikianza vizuri wakishambulia kujaribu kutafuta mabao ya kusawazisha, lakini safu ya ulinzi ya Simba chini ya kipa Aishi Salum Manula ilisimama imara.
Kibao kikaigeukia Mbao FC na wakajikuta wanapachikwa mabao matatu ndani ya dakika 20, Okwi akianza kufunga dakika ya 69 kwa shuti la mguu wa kulia baada ya kupokea pasi ya Muzamil Yassin.
Okwi anatolewa nje anachechemea baada ya kuumia kufuatia kugongana na beki wa Mbao FC, Amos Charles kwenye boksi na nafasi yake kuchukuliwa na Mrundi, Laudit Mavugo.   
Beki mkongwe anayeweza kucheza kama kiungo pia, Erasto Edward Nyoni akaifungia Simba SC bao la nne dakika ya 82 kwa shuti la mpira wa adhabu kutoka umbali wa mita 19 kasoro kidogo, baada ya Muzamil kuangushwa.
Refa Onoka akamtoa nje kwa nyekundu Nahodha wa Mbao FC, Ndikumana dakika ya 84 baada ya kumuonyesha kadi ya pili ya njano kufuatia kumchezea rafu Mavugo Mrundi mwenzake, Mavugo.
Nicholaus Gyan akaifungia Simba SC bao la tano dakika ya 86 kufuatia krosi ya beki wa kulia, Shomary Kapombe kuzua kizaazaa langoni kwa Mbao FC. 
Kikosi cha Simba SC; Aishi Manula, Shomari Kapombe, James Kotei, Yussuph Mlipili, Erasto Nyoni, Asante Kwasi, Jonas Mkude, Said Ndemla, Shiza Kichuya/Rashid Juma dk86, Nicholas Gyan na Emmanuel Okwi/Laudit Mavugo dk80.
Mbao FC; Iyvan Rugumandiye, Boniphace Maganga, Amos Charles, David Mwasa, Yusuph Ndikumana, Ibrahim Njohole/ Said K. Said dk57, Herbet Lukindo, George Sangija, Habibu Hajji, James Msuva/Rajesh Kotecha dk51 na Emmanuel Mvuyekure/Ismail Ally dk70.

YANGA AHUENI MAANDALIZI LIGI YA MABINGWA, YAAHIRISHA MECHI NA MTIBWA

MCHEZO wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya wenyeji Mtibwa Sugar na Yanga SC ya Dar es Salaam uliopangwa kufanyika Machi 3, mwaka huu Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro umeahirishwa. 
Sababu za kuuahirisha mchezo huo namba 170 ni kuipa Yanga nafasi nzuri ya maandalizi ya mchezo wake wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers ya Botswana Machi 6 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Busara za Bodi chini ya Mwenyekiti wake, Clement Sanga ambaye pia ni Kaimu Mwenyekiti wa Yanga SC zimeielekeza kuusogeza mbele mchezo wa Ligi Kuu ili kuwapa wawakilishi hao wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa fursa nzuri ya maandalizi. 

Baada ya kukata tiketi ya Robo Fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) kufuatia ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Maji Maji Uwanja wa Maji Maji mjini Songea Jumapili, Yanga iliondoka mjini humo mapema Jumatatu kwa basi lake kwenda Mtwara tayari kwa mchezo mwingine wa Ligi Kuu dhidi ya wenyeji, Ndanda FC Jumatano Uwanja wa Nangwanda Sijaona.
Mabao ya Yanga Jumapili yalifungwa na kiungo Pius Charles Buswita kwa kichwa dakika ya 40 akimalizia krosi ya beki Mwinyi Hajji Mngwali kutoka upande wa kushoto baada ya kuanzishiwa kona fupi na kiungo mwenzake, waliyekuwa wakicheza naye pale mbele, Ibrahim Ajib na winga Emmanuel Martin dakika ya 57 akimalizia kwa kichwa krosi ya beki wa kulia, Hassan Kessy aliyemlamba chenga Mpoki Mwakinyuki.
Bao pekee la Maji Maji lilifungwa na kiungo Jaffar Mohammed kwa kichwa dakika ya 61, akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na beki Aziz Sibo kufuatia Nahodha, Kevin Yondan kumchezea rafu Marcel Boniventura.
Yanga ilikata tiketi ya kwenda Raundi ya Kwanza ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika Jumatano iliyopita licha ya sare ya 1-1 na wenyeji, Saint Louis Suns United katika mchezo wa marudiano wa Raundi ya Awali Uwanja wa Linite.
Mabingwa hao wa Tanzania wamesonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 2-1 baada ya Februari 10 kushinda 1-0 pia Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, bao pekee la kiungo Juma Mahadhi aliyekosekana uwanjani kwenye mechi ya marudiano kwa sababu ya homa.
Kwa kuitoa St Louis, Yanga itakutana na Township Rollers ya Botswana katika Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ambayo nayo iliitoa El Merreikh ya Sudan, mechi ya kwanza ikichezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Machi 6 kabla ya kwenda Gaborone kwa mchezo wa marudiano, Machi 17.

Saturday, January 27, 2018

Real madrid yaicha 4-1 valencia


Cristiano Ronaldo (kulia) akishangilia na wenzake kumpongeza Marcelo baada ya kuifungia Real Madrid bao la tatu dakika ya 84 katika ushindi wa 4-1 dhidi ya wenyeji, Valencia kwenye mchezo wa La Liga leo Uwanja wa Mestalla. Ronaldo naye alifunga mabao mawili, yote kwa penalti dakika za 16 na 38 wakati bao la nne limefungwa na Toni Kroos dakika ya 89, huku la Valencia likifungwa na Santi Mina dakika ya 58

Morocco na Sudan zatinga nusu fainali CHAN



WENYEJI, Morocco na Sudan wamefanikiwa kwenda Nusu Fainali za michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) baada ya ushindi dhidi ya Namibia na Zambia usiku wa jana.