SIMBA
SC imezidi kuukimbilia kwa kasi ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara baada ya ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Mbao FC ya Mwanza jioni ya jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mshambuliaji
Mganda, Emmanuel Okwi alifunga mabao mawili moja kila kwa kipindi kabla
ya kuumia na kutolewa wakati mabao mengine yalifungwa na Shiza Kichuya,
Erasto Nyoni na Mghana, Nicholaus Gyan.
Ushindi
huo unaifanya Simba itimize pointi 45 baada ya kucheza mechi 19,
ikiendelea kukaa kileleni mwa Ligi Kuu, ikifuatiwa na mabingwa watetezi,
Yanga wenye pointi 37 za mechi 18, wakati Mbao FC inabaki nafasi ya 10
kwa pointi zake 19 za mechi 19.
li
kuanza kupata mabao, benchi la Ufundi la Simba chini ya kocha Mfaransa,
Pierre Lechantre anayesaidiwa na Mrundi, Masoud Juma lililazimika
kufanya mabadiliko ya mapema kipindi cha kwanza katika safu ya kiungo
kwa kumtoa Said Hamisi Ndemla na kumuingiza Muzamil Yassin baada ya nusu
saa.
Mabadiliko
hayo yalibadilisha kabisa mwelekeo wa mechi, kutoka Mbao FC kutawala
hadi Simba SC ambayo wiki ijayo itamenyana na El Masry ya Misri katika
Raundi ya Kwanza ya kombe la Shirikisho Afrika kuuteka mchezo.
Shiza
Ramadhani Kichuya akafungua sherehe za mabao za Simba kwa kufunga bao
la kwanza dakika ya 38 akimalizia pasi ya mtokea benchi, Muzamil.
Mganda
Emmanuel Okwi akaifungia Simba SC bao la pili dakika ya 40 kwa penalti,
baada ya yeye mwenyewe kuanguka kwenye boksi wakati anadhibitiwa na
beki wa Mbao, David Mwasa.
Refa
Erick Onoka kutoka Arusha akawanyima Simba SC penalti sahihi zaidi ya
aliyowapa mwanzo baada ya Okwi kuangushwa kwenye boksi na Nahodha wa
Mbao FC, Mrundi, Yusuph Ndikumana ambaye leo alicheza chini ya kiwango.
Kipindi
cha pili, Mbao FC wanaofundishwa na kocha Mrundi, Etienne Ndayiragijje
walikianza vizuri wakishambulia kujaribu kutafuta mabao ya kusawazisha,
lakini safu ya ulinzi ya Simba chini ya kipa Aishi Salum Manula
ilisimama imara.
Kibao
kikaigeukia Mbao FC na wakajikuta wanapachikwa mabao matatu ndani ya
dakika 20, Okwi akianza kufunga dakika ya 69 kwa shuti la mguu wa kulia
baada ya kupokea pasi ya Muzamil Yassin.
Okwi
anatolewa nje anachechemea baada ya kuumia kufuatia kugongana na beki
wa Mbao FC, Amos Charles kwenye boksi na nafasi yake kuchukuliwa na
Mrundi, Laudit Mavugo.
Beki
mkongwe anayeweza kucheza kama kiungo pia, Erasto Edward Nyoni
akaifungia Simba SC bao la nne dakika ya 82 kwa shuti la mpira wa adhabu
kutoka umbali wa mita 19 kasoro kidogo, baada ya Muzamil kuangushwa.
Refa
Onoka akamtoa nje kwa nyekundu Nahodha wa Mbao FC, Ndikumana dakika ya
84 baada ya kumuonyesha kadi ya pili ya njano kufuatia kumchezea rafu
Mavugo Mrundi mwenzake, Mavugo.
Nicholaus
Gyan akaifungia Simba SC bao la tano dakika ya 86 kufuatia krosi ya
beki wa kulia, Shomary Kapombe kuzua kizaazaa langoni kwa Mbao FC.
Kikosi
cha Simba SC; Aishi Manula, Shomari Kapombe, James Kotei, Yussuph
Mlipili, Erasto Nyoni, Asante Kwasi, Jonas Mkude, Said Ndemla, Shiza
Kichuya/Rashid Juma dk86, Nicholas Gyan na Emmanuel Okwi/Laudit Mavugo
dk80.
Mbao
FC; Iyvan Rugumandiye, Boniphace Maganga, Amos Charles, David Mwasa,
Yusuph Ndikumana, Ibrahim Njohole/ Said K. Said dk57, Herbet Lukindo,
George Sangija, Habibu Hajji, James Msuva/Rajesh Kotecha dk51 na
Emmanuel Mvuyekure/Ismail Ally dk70.
No comments:
Post a Comment