MCHEZO
wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya wenyeji Mtibwa Sugar na
Yanga SC ya Dar es Salaam uliopangwa kufanyika Machi 3, mwaka huu Uwanja
wa Jamhuri mjini Morogoro umeahirishwa.
Sababu
za kuuahirisha mchezo huo namba 170 ni kuipa Yanga nafasi nzuri ya
maandalizi ya mchezo wake wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township
Rollers ya Botswana Machi 6 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Busara
za Bodi chini ya Mwenyekiti wake, Clement Sanga ambaye pia ni Kaimu
Mwenyekiti wa Yanga SC zimeielekeza kuusogeza mbele mchezo wa Ligi Kuu
ili kuwapa wawakilishi hao wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa fursa
nzuri ya maandalizi.
Baada
ya kukata tiketi ya Robo Fainali ya michuano ya Azam Sports Federation
Cup (ASFC) kufuatia ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Maji Maji Uwanja wa
Maji Maji mjini Songea Jumapili, Yanga iliondoka mjini humo mapema
Jumatatu kwa basi lake kwenda Mtwara tayari kwa mchezo mwingine wa Ligi
Kuu dhidi ya wenyeji, Ndanda FC Jumatano Uwanja wa Nangwanda Sijaona.
Mabao
ya Yanga Jumapili yalifungwa na kiungo Pius Charles Buswita kwa kichwa
dakika ya 40 akimalizia krosi ya beki Mwinyi Hajji Mngwali kutoka upande
wa kushoto baada ya kuanzishiwa kona fupi na kiungo mwenzake,
waliyekuwa wakicheza naye pale mbele, Ibrahim Ajib na winga Emmanuel
Martin dakika ya 57 akimalizia kwa kichwa krosi ya beki wa kulia, Hassan
Kessy aliyemlamba chenga Mpoki Mwakinyuki.
Bao
pekee la Maji Maji lilifungwa na kiungo Jaffar Mohammed kwa kichwa
dakika ya 61, akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na beki Aziz Sibo
kufuatia Nahodha, Kevin Yondan kumchezea rafu Marcel Boniventura.
Yanga
ilikata tiketi ya kwenda Raundi ya Kwanza ya michuano ya Ligi ya
Mabingwa Afrika Jumatano iliyopita licha ya sare ya 1-1 na wenyeji,
Saint Louis Suns United katika mchezo wa marudiano wa Raundi ya Awali
Uwanja wa Linite.
Mabingwa
hao wa Tanzania wamesonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 2-1 baada ya
Februari 10 kushinda 1-0 pia Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, bao pekee
la kiungo Juma Mahadhi aliyekosekana uwanjani kwenye mechi ya marudiano
kwa sababu ya homa.
Kwa
kuitoa St Louis, Yanga itakutana na Township Rollers ya Botswana katika
Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ambayo nayo iliitoa El
Merreikh ya Sudan, mechi ya kwanza ikichezwa Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam Machi 6 kabla ya kwenda Gaborone kwa mchezo wa marudiano, Machi
17.
No comments:
Post a Comment