![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEihyphenhyphen8nKxwbTntRYHX_Ovf55JZhEJDQL75fktuFCVeZX7iwO1obTZaHBylkEMtF79p-z_-SJeoAQ9XYxxJfMpcWCwyV_feFpkM4Lm9Lw9JuZBSiXF1p08kpuvj9bL3vMtodbCc5yca9PZh7d/s400/49800DB400000578-0-image-m-36_1519679475884.jpg)
KLABU ya Arsenal itaitathmini nafasi ya Arsene Wenger mwishoni mwa msimu — kukiwa na uwezekano wa kuhitimisha miaka 22 ya Mfaransa huyo.
The Gunners tayari
wamekwishaanza kuandaa orodha ya makocha wa kuwatathmini katika kumpata
mbadala wa Wenger kama itaamua kuachana naye mwishoni mwa msimu.
Kocha wa Monaco, Leonardo Jardim, kocha wa Ujerumani, Joachim
Low, kocha Mkuu wa Celtic, Brendan Rodgers na kocha wa Manchester City,
Mikel Arteta ni miongoni mwa watu awali walioorodheshwa.
Vyanzo
vinasema kwamba Wenger, ambaye nafasi yake iko hatarini baada ya kipigo
cha Jumapili katika fainali ya Carabao Cup kutoka kwa Manchester City,
atalazimika kupambana ili kumalizia miezi yake 12 ya mkataba wake.
Lakini inavyoonekana sasa ndani ya Arsenal nguvu ya kumng'oa Wenger klabu hiyo ya Kaskazini mwa London mwishoni mwa msimu.
Tathmini ya mwishoni mwa msimu ndio itabeba mustakabali wa Wenger kama apewe nafasi nyingine ya kubaki kwa msimu mwingine au aondolewe. Hii inamuacha apambane maswali magumu juu ya nini amevuna katika msimu hadi sasa.
Zaidi itategemea kama ataiwezesha timu kupata nafasi ya kurejea kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu, ingawa hiyo bado haitatosha kuwa sababu ya kumbakiza.
Na safari ya kurejea kwenye michuano hiyo mikubwa ya Ulaya inaonekana kuwa ngumu, kwa sasa The Gunners wakizidiwa pointi 10 na Tottenham Hotspur wanaoshika nafasi ya nne.
Hivyo, nafasi nzuri zaidi ya Arsenal kurejea kwenye michuano hiyo kwa kushinda taji la UEFA Europa League, ingawa wanakabiliwa na mtihani mgumu wa kumenyana na AC Milan katika raundi ijayo, hatua ya 16 Bora.

No comments:
Post a Comment