Sunday, December 10, 2017

Liverpool kutengeneza rekodi leo mbele ya Everton



Kabla ya mchezo kati ya Manchester United vs Manchester City dunia itashuhudia mchezo mkubwa mwingine nchini Uingereza ambapo majogoo wa London Liverpool watakuwa nyumbani kuikaribisha Everton.

Kama hii leo Liverpool wataibuka kidedea vs Everton basi watakuwa wameifikia rekodi yao ya kucheza na Everton michezo 15 bila kupoteza mchezo hata mmoja mbele ya wapinzani wao wakubwa

Ushindi wa bao 1 kwa 0 katika uwanja wa Anfield mwaka 1999 ndio ulikuwa ushindi wao wa mwisho kwa Everton kuibuka na ushindi katika uwanja wa Anfield na tangu kipindi hicho hawajawahi kushinda Anfield.

Lakini Everton wanakabiliwa na wakati mgumu zaidi mbele ya Liverpool kwani katika michezo 21 iliyopita kati ya Everton na Liverpool, Everton wamefanikiwa kuibuka na ushindi mara 1 tu,wakipigwa mara 11 na suluhu 9.

Lakini kama ulikuwa hujui  ni kwamba mchezo kati ya Liverpool na Everton ndio mchezo unaoongoza kwa kutoa kadi nyekundu EPL (21) katika mechi 50 huku Everton wakipata kadi 14 na Liverpool wakipata 7.

Liverpool wanaonekana kucheza kwa uelewano sana wanapokuwa nyumbani kwani katika michezo waliyocheza wameruhusu mabao mawili tu Anfield huku wakiwa hawajafungwa katika mechi 6 Epl.

No comments:

Post a Comment