Wapenda soka wengi nchini wameonekana
kukerwa na kikosi cha Kilimanjaro Stars kilichoshiriki michuano ya
Chalenji inayoendelea nchini Kenya.
Hata hivyo, kero hiyo imezidi kuwa kubwa
baada ya Kocha Mkuu wa Kilimanjaro Stars, Ammi Ninje kusema “always
next time”, akimaanisha wakati mwingine baada ya Stars kushindwa kufanya
vizuri katika michuano hiyo.
Jana mchana, Stars imefungwa kwa mabao 2-1
na Rwanda ikiwa imetangulia kufunga baadaye Amavubi wakasawazisha na
kupata bao la ushindi.
Kili Stars inafungwa mechi ya pili
mfululizo baada ya kuwa imelala kwa mabao 2-1 kutoka kwa Zanzibar Heroes
ambao walianza kwa kufungwa, wakasawazisha na kupata ushindi.
Wakati akihojiwa, Ninje alionekana ni mchangamfu, akisifia vijana wake walivyocheza na kuongeza kwamba “until next time”.
Mashabiki wa soka wamekuwa wakijadili
uwezo wake na baadhi wanaeleza kwamba Uingereza alifundisha timu za
watoto na hakuwa na nafasi ya kufundisha timu ya taifa.
Wako ambao wanamtetea ambao ni idadi ndogo na kundi la tatu la mjadala ni lile linalowachambua wachezaji kutoonyesha juhudi.
No comments:
Post a Comment