KLABU
Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imetoka sare ya bao 1-1 na
Friends Ranger katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa
Azam Complex usiku wa jana.
Ilikuwa
ni siku nzuri kwa mshambuliaji mpya wa timu hiyo Bernard Arthur,
aliyekuwa akicheza mechi yake ya kwanza tokea asajiliwe akitokea Liberty
Professional ya Ghana baada ya kufunga bao la kusawazisha dakika ya 68.
Mpira
huoa ulikuwa ni mkali sana ambapo Azam FC ilicheza vema kipindi cha
pili baada ya mabadiliko ya kuingia winga Enock Atta, kiungo Frank
Domayo na mshambuliaji Wazir Junior.
Friends
Ranger ilijipatia bao lake dakika ya 65 kupitia kwa Mau Gola kufuatia
uzembe uliofanyika kwenye safu ya ulinzi ya Azam FC kabla ya dakika tatu
baadaye matajiri hao kusawazisha.
Azam
FC iliutumia mchezo huo kama sehemu ya kuwapa ushindani wachezaji wake
kutokana na kusimama kwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) kupisha
michuano ya Kombe la Chalenji inayoendelea nchini Kenya.
Kikosi cha Azam FC jana kilikuwa; Mwadini
Ally, Swaleh Abdallah, Hamimu Abdallah/Daniel Amoah dk 76, David
Mwantika, Agrey Moris/Oscar Masai dk 86, Salmin Hoza, Braison
Raphael/Enock Atta dk 66, Masoud Abdallah/Frank Domayo dk 61, Ramadhan
Singano/Wazir Junior dk 61, Bernard Arthur/Paul Peter dk 70, Joseph
Mahundi
No comments:
Post a Comment