![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhxG9Yhtyej4yFiMHsMmvyeNdshJy-StkeYNoG8XIfXvU54Vks-_-GxgHb3Xq_-d3fzi-5JnRMrbvAW-f8Z5AUxABK8q4jQkbnfP3Lk1w7nRlsnFNlIKsbZLy3a_i6-Yy2udV4SWcxoKQQ/s400/BENDERA+%2523salehjembe.jpg)
Viongozi
wakuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Rais Wallace
Karia na Makamu Rais Michael Wambura wataongoza ujumbe wa shirikisho
katika mazishi Kocha wa zamani wa Taifa Stars, marehemu Joel Nkaya
Bendera.
Bendera
aliyefariki dunia Desemba 6, mwaka huu kwenye Hospitali ya Taifa
Muhimbili, atazikwa leo Jumapili Desemba 10, 2017 makaburi ya Kijiji cha
Manundu, Korogwe mkoani Tanga.
Ujumbe
huo pia utamjumuisha Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini la TFF, Mhe.
Mohammed Abdulaziz; Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi;
Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi, Vedastus Lufano pamoja na Mjumbe wa
Kamati ya Utendaji wa Kanda ya 12 (Mikoa ya Tanga na Kilimanjaro),
Khalid Mohammed.
Khalid
Mohammed atakuwa na wenyeji wengine ambao ni viongozi wa mpira wa miguu
mkoa na wilaya za Tanga ambao wataungana familia pamoja na waombolezaji
wengine kumpumzisha Mbunge huyo wa zamani wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania (1995 hadi 2005) katika Jimbo la Korogwe Mjini.
Mwili
wa marehemu Bendera umeagwa Jumamosi Desemba 9, mwaka huu asubuhi
kwenye Viwanja vya Hospitali ya Jeshi la Lugalo, Dar es Salaam.
Enzi
zake Joel Nkaya Bendera alifikia cheo cha Naibu Waziri Michezo mbali ya
kuongoza mikoa ya Morogoro na Manyara kwa cheo cha Mkuu wa mkoa.
Anakumbukwa
zaidi kuwa sehemu ya benchi la ufundi lenye mafanikio kuingoza timu ya
soka ya Tanzania kuiondoa Zambia na Tanzania kufuzu kwa fainali za Kombe
la Mataifa Huru ya Tanzania mwaka 1979.
Taifa
Stars ilishinda bao 1-0 dhidi ya KK Eleven ya Zambia (sasa Chipolopolo)
na kuifanya Tanzania kushiriki kwa mara ya kwanza michuano hiyo mikubwa
Afrika kwa upande wa timu za taifa iliyofanyika Nigeria. Taifa Stars
haijafuzu tena katika michuano hiyo.
Joel
Bendera – ndiye aliyeiongoza Simba kushinda mabao 5-0 dhidi ya Mufulira
Wondereres huko Zambia katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka
1979.
Ikumbukwe kwamba Simba ilifungwa mabao 4-0 katika mchezo wa kwanza ulifanyika Dar es Salaam.
Joel
Bendera – ndiye aliyeiongoza Coastal Union ya Tanga kutwaa ubingwa wa
Bara na kucheza michuano ya Afrika Mashariki na Kati na kuifikisha timu
hiyo fainali. Wakati akifanya kazi na hayati Zacharia Kinanda.
Joel
Bendera – akiwa Naibu Waziri Michezo, chini Waziri George Huruma
Mkuchika ndiye aliyeihamaisha Taifa Stars kucheza vema hadi kufuzu kwa
fainali za Kombe la Mataifa ya kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN), mwaka
2009.
No comments:
Post a Comment