Saturday, January 27, 2018

SIMBA KUTANDAZA SOKA SAFI MBELE YA MFARANSA LEO

 Image result for kikosi cha simba picha 
RAUNDI ya kwanza ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inahitimishwa leo kwa michezo miwili, vinara Simba SC wakiwakaribisha Maji Maji ya Songea

Saturday, January 20, 2018

Uganda yatupwa nje CHAN


 TIMU ya Taifa ya Uganda imetolewa kwenye michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN),

safari ya Ndemla ziiiiiii


KIUNGO wa Simba, Said Ndemla, sasa anajiandaa kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuwepo Msimbazi huku ikielezwa lile dili la kwenda kucheza Ulaya limeyeyuka.
Ndemla ambaye mkataba wake wa sasa na Simba unamalizika Aprili, mwaka huu, mwishoni mwa mwaka jana alikwenda Sweden kufanya majaribio kwenye timu ya AFC Eskelistuna na kufuzu.

Hata hivyo, licha ya kufuzu majaribio hayo, Ndemla ameshindwa kujiunga na timu hiyo.
Taarifa kutoka ndani ya Simba zinasema kuwa, uongozi umeridhishwa na kiwango cha Ndemla, hivyo wameona bora waendelee kuwa naye ili kukiongezea nguvu kikosi katika mechi za Kombe la Shirikisho Afrika.

“Mkataba wake unaelekea ukingoni lakini wakati wowote anaweza kuongezewa kwa sababu uongozi unaridhishwa na kiwango chake ukizingatia kwamba tuna michuano ya kimataifa.
“Hii inamaanisha kuwa, huu si wakati wa kuacha wachezaji kama yeye,” kilisema chanzo hicho.

Alipotafutwa meneja wa mchezaji huyo, Jamal Kisongo kuzungumzia mustakabali wa Ndemla, alisema: “Lile dili lake kule Sweden tumewaachia Simba waamue kwani bado ni mchezaji wao, vyovyote watakavyosema ni sawa hakuna shida.”

Wakati hayo yakijiri, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amemuahidi kiungo huyo kumpatia gari kutokana na kiwango chake bora alichokionyesha msimu huu

Ujio wa Pierre-Emerick Aubameyang Arsenal ni dawa


Straika Pierre-Emerick Aubameyang kutoka Borussia Dortmund ya Ujerumani.
LONDON, England
ARSENAL chini ya kocha wake Arsene Wenger inapambana kuhakikisha inamsajili straika Pierre-Emerick Aubameyang kutoka Borussia Dortmund ya Ujerumani.
Aubameyang raia wa Gabon anatakiwa na Arsenal kwa udi na uvumba ili kuziba nafasi ya straika Alexis Sanchez ambaye anatarajiwa kujiunga na Manchester United au Manchester City.
Maisha ya Aubameyang katika Klabu ya Borussia Dortmund sasa siyo mazuri na inaonekana wazi straika huyo anataka kuondoka na klabu iliyoonyesha nia ya kumsajili ni Arsenal.
Wenger hana jinsi zaidi ya kumuachia Sanchez kwenda jijini Manchester kwani isipofanya hivyo sasa, inaweza kumtoa bure katika usajili ujao kabla ya msimu mpya.
Hata hivyo zipo sababu zinazoonyesha kuwa, Aubameyang anaweza kuisumbua Arsenal kutokana na sababu zifuatazo:
#5 Kulazimisha ushindi
Aubameyang anajua kufunga na akiwa karibu na lango ni mtu hatari sana kwa wapinzani. Hata hivyo, ana tatizo la kutokuwa mpambanaji kwa ajili ya timu na hana njia nyingi za kuwabuguzi mabeki, akishindwa njia moja ndiyo basi tena. Anategemea kufunga kwa kutengenezewa nafasi na wakishindwa kumfanyia hivyo ndiyo basi tena.

#4 Tatizo la ulinzi
Moja kati ya matatizo makubwa ya Aubameyang awapo uwanjani ni mchango wake wa kukaba. Kwa soka la sasa hasa England, kukaba ni kazi ya mshambuliaji pia ili kupunguza kasi ya adui. Sasa Aubameyang yeye si mzuri katika kukaba hivyo atapata tabu katika mfumo huo.

#3 Hayupo kama zamani
Aubameyang wa sasa si yule wa msimu mmoja au miwili nyuma, ameshuka pia vituko vyake nje ya uwanja ni tatizo kichwani mwake. Sawa, sasa anaweza kuwa amefunga mabao 21 katika mechi 23 msimu huu, lakini hailingani na nafasi anazopoteza uwanjani sasa katika kikosi cha Borussia Dortmund.
#2 Gharama yake haiendani na umri
Aubameyang sasa ana umri wa miaka 28, hivyo dau la Borussia Dortmund la kumuuza kwa pauni milioni 53 (Sh bilioni 162.8), haiwezi kuwa na faida kwao kwani hatoweza kucheza kwa ushindani kwa muda mrefu. Hii ina maana kuwa, Arsenal haitaweza kumtumia kwa muda mrefu.

#1 Hawezi kuwa Alexis Sanchez
Ukweli ni kwamba, Aubameyang hawezi kuwa mbadala sahihi wa Alexis Sanchez. Arsenal inadhani Aubameyang ndiye mbadala sahihi wa Sanchez lakini ukweli ni kwamba wawili hao wapo tofauti kabisa. Aubameyang anacheza kwa mtindo mmoja na kwa kutumia upande mmoja tu lakini Sanchez yupo pande zote. Hapa ndipo Arsenal inapoongeza nguvu pia kumnasa Malcom wa Bordeaux.

Beno Kakolanya hatimaye amerejea mazoezini Yanga.


Baada ya mgomo wa muda wa takribani wiki mbili, kipa Beno Kakolanya hatimaye amerejea mazoezini Yanga.

Kakolanya amerejea na kuendelea na mazoezi na wenzake kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kuendelea kujiandaa na mechi zijazo za Ligi Kuu Bara.

Kipa huyo mzoefu aliyejiunga na Yanga akitokea Prisons ya Mbeya, aliweka mgomo akitaka kumaliziwa fedha alizokuwa anadai.

Hata hivyo, ilionekana uongozi wa Yanga ulikuwa ukipambana kumrejesha Obrey Chirwa ambaye pia aligomea kwao Zambia kutokana na kutolipwa fedha zake pia.


Baadaye, uongozi huo ulifanikiwa kumrekesha Chirwa timu ikiwa kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi na sasa Kakolanya naye amerejea.

ngoma awatembelea wachezaji wenzake mazoezini

Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma bado ni majeruhi na hajajiunga na wenzake.

Lakini jana aliamua kuwatembelea wenzake mazoezini kwenye Uwanja wa Uhuru wakati wakiendelea kujifua kujiandaa na mechi za Ligi Kuu Bara.

Raia huyo wa Zimbabwe, ameendelea kukaa nje kwa zaidi ya miezi miwili sasa na imekuwa zaidi ya wiki tatu tokea arejee Dar es Salaam akitokea kwao Zimbabwe ambako ilielezwa amekwenda kupata matibabu nchini Afrika Kusini.
 

Beki kisiki wa kati wa Yanga,nje dhidi ya Ruvu Shooting

Beki kisiki wa kati wa Yanga, Kelvin Yondani anatarajiwa kuikosa mechi ya kesho dhidi ya  ya Ligi Kuu Bara itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Yondani ataikosa mechi hiyo kutokana na kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano alizozipata kwenye mechi zilizopita za ligi kuu.

Kutokana na hali hiyo, timu inaweza kumtumia beki wa kati Nadir Haroub ‘Cannavaro’ au Said Makapu kucheza nafasi hiyo ya beki ya kati pamoja na Vicent Andrew ‘Dante’.

Taarifa zinaeleza Benchi la Ufundi la Yanga tayari limeanza kuchukua tahadhari ya kuwaandaa baadhi ya wachezaji akiwemo Cannavaro atakayecheza nafasi ya Yondani.

“Yondani ameondolewa kwenye mipango ya kocha katika kuelekea mechi dhidi ya Ruvu itakayochezwa Jumapili Uwanja wa Taifa.

“Beki huyo ataukosa mchezo huo kutokana na kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano alizozipata katika michezo iliyopita ya ligi kuu,” alisema mtoa taarifa huyo.


Meneja Mkuu wa Yanga, Hafidh Saleh alithibitisha Yondani kuondolewa kikosini; “Ni kweli Yondani hatakuwepo katika mechi dhidi ya Ruvu kwani ana adhabu ya kadi tatu za njano.”