Saturday, November 18, 2017

WELBECK YUPO FITI KUIKABIRI SPURS LEO

 


















Mshambuliaji Danny Welbeck akimruka kipa Petr Cech anayedaka mpira chini wakati wa mazoezi ya Arsenal jana viwanja vya Colney,

Singida United imepanda kwa nafasi moja

TIMU ya Singida United imepanda kwa nafasi moja hadi ya tano baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Lipuli ya Iringa kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya Jana Uwanja wa Namfua, Singida.

MAHASIMU WA MADRID LEO

 












Mshambuliaji Cristiano Ronaldo akionekana mwenye kujiamini wakati wa mazoezi ya Real Madrid jana katika viwanja vyao vya mazoezi vya Valdebebas mjini Madrid, Hispania kujiandaa na mchezo wa leo wa La Liga dhidi ya Atletico Madrid Uwanja wa Wanda Metropolitano mjini Madrid

Dortmund yalala 2-1 dhidi ya Stuttgart.


Ikiwa inacheza mechi yake ya 12 ya Bundesliga, Borussia Dortmund imepoteza mchezo wake wa nne.

Dortmund ikicheza bila ya mshambulizi wake nyota, Pierre-Emerick Aubameyang imepigwa 2-1 dhidi ya Stuttgart.

Mechi hiyo ilikuwa inarushwa moja kwa moja kupitia king'amuzi cha StarTimes kinachoshika umaarufu mkubwa kwa sasa katika masuala ya michezo.

Hali hiyo inaofanya Dortmund kubaki katika nafasi ya tatu nyuma ya vinara wa Bundelisga kwa sasa, Bayern Munich wanaofuatiwa na RB Leipzig.

Haiwezekani hata kidogo Tambwe kuwa Mfungaji Bora....Kichuya

Kila mtu anakuwa na mawazo yake katika jambo fulani, lakini kiungo nyota wa Simba, Shiza Kichuya anaweza kutofautiana na wengi sana kuhusiana na Amissi Tambwe wa Yanga.

IRENE UWOYA KUHANI MSIBA WA NDIKUMANA KIGALI

rembo wa zamani wa taji la Miss Chang’ombe na mwigizaji maarufu nchini, Irene Uwoya amewasili jijini Kigali, Rwanda kuhani msiba wa aliyekuwa mumewe, Ndikumana Hamad.

Sunday, November 12, 2017

Uwanja wa Taifa kukamilika November 21


Jana November 11, 2017 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akiambatana na kamati ya maandalizi ya fainali za Afrika (AFCON U17) amefanya ziara ya kutembelea uwanja wa taifa kukagua ukarabati unaoendelea katika eneo la kuchezea (pitch) na maeneo mengine.
Dkt. Mwakyembe ameishukuru kampuni ya SportPesa ambayo ndio imebeba jukumu la kukarabati uwanja huo.



“Nashukuru kuona nyasi za uwanjani zimeota vizuri na unapendeza, kikubwa nashukuru kwa vijana wetu sita ambao wamefundishwa namna ya kutunza viwanja”-Dkt. Mwakyembe.

Mkuu wa oparesheni SportPesa Luca Neghesti amethibitisha ukarabati wa uwanja utakamilika November 21 na utakabidhiwa November 24 mwaka huu ukiwa tayari kwa matumizi.
“Kazi ya kukarabati sehemu ya kuchezea imekamilika na nyasi zilizooteshwa zimeota vizuri na zimeshika hivyo upo tayari kutumika,” alisema Luca.

Vilabu vya Simba na Yanga ambavyo huutumia uwanja wa taifa kwa mechi zao za nyumbani huenda zikarejea kwenye uwanja huo kuanzia November 24 baada ya kukabidhiwa kwa serikali. Vilabu hivyo vililazimika kutumia uwanja wa Uhuru kwa mechi zao za nyumbani kupisha matengenezo yanayoendelea uwanja wa Taifa.