Saturday, November 18, 2017

Dortmund yalala 2-1 dhidi ya Stuttgart.


Ikiwa inacheza mechi yake ya 12 ya Bundesliga, Borussia Dortmund imepoteza mchezo wake wa nne.

Dortmund ikicheza bila ya mshambulizi wake nyota, Pierre-Emerick Aubameyang imepigwa 2-1 dhidi ya Stuttgart.

Mechi hiyo ilikuwa inarushwa moja kwa moja kupitia king'amuzi cha StarTimes kinachoshika umaarufu mkubwa kwa sasa katika masuala ya michezo.

Hali hiyo inaofanya Dortmund kubaki katika nafasi ya tatu nyuma ya vinara wa Bundelisga kwa sasa, Bayern Munich wanaofuatiwa na RB Leipzig.

No comments:

Post a Comment