TIMU
ya taifa ya Morocco imekata tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia
mwakani nchini Urusi baada ya kuwapiga wenyeji, Ivory Coast mabao 2-0
mjini Abidjan.
Simba
wa Atlas waliingia kwenye mechi hiyo Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny
wakiwa wanawazidi pointi moja Tembo wa Ivory Coast na walihitaji sare tu
ili kupata nafasi ya kwenda Urusi mwakani.
Hata
hivyo, mabao mawili ndani ya dakika tano kutoka kwa Nabil Dirar na
Medhi Benatia yaliwapa ushindi mzuri katika mechi hiyo ya Kundi C.
Winga
wa Fenerbahce, Dirar aliifungia Morocco bao la kwanza dakika ya 25
baada ya krosi yake kutoka upande wa kulia kuingia moja kwa moja kwenye
nyavu za Ivory Coast.
Nahodha Medhi Benatia akafunga bao la pili kiulaini dakika ya 30.
Ivory
Coast ilpata nafasi kadhaa za kufunga mabao, lakini ikashindwa
kuzitumia vizuri ikiwemo ya beki wa Tottenham, Serge Aurier aliyepiga
juu ya lango kipindi cha pili.
Matokeo
hayo yanaifanya timu ya Marc Wilmots, Ivory Coast ikose fainali za
Kombe la Dunia mwakani, maana yake majina makubwa ya nyota wa timu hiyo
wanaocheza Ligi Kuu ya England kama Wilfried Zaha, Serge Aurier na Eric
Bailly yatakakuwa mapumzikoni katikati ya mwakani.
Morocco
inaungana na Tunisia kukamilisha nchi tano za Afrika zilizofuzu Kombe
la Dunia, nyingine zikiwa ni Nigeria, Misri na Senegal.
Ushindi
huom, unamfanya kocha Herve Renard awaumize waajiri wake wa zamani,
timu ambayo aliiongoza kutwaa Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2015.
Morocco
imefuzu siyo tu bila kupoteza mechi, ikishinda mechi tatu na kutoa sare
tatu, pia imeruhusu nyavu zake kutikisika mara moja tu.
Renard
anasaidiwa na Mwanasoka Bora wa zamani wa Afrika, Mustapha Hadji,
kiungo wa zamani wa Morocco na klabu za Coventry na Aston Villa.
Kikosi
cha Ivory Coast kilikuwa: Gbohouo, Aurier, Gbamin, Kanon, Deli/Konan
dk45, Fofana/Cornet dk62, Gradel, Kessie, Zaha, Doumbia na
Gervinho/Kalou dk76.
Morocco:
Mohamedi, Dirar, Benatia, Saiss, Hakimi, Boussoufa, El Ahmadi,
Belhanda/Fajr dk90+1, Ziyech/S Amrabat dk82, Boutaib/Bencharki dk75 na N
Amrabat.
No comments:
Post a Comment