Mchezo wa pili kati ya michezo kumi iliyopita Pep Gurdiola anapata
ushindi zidi ya Arsenal ushindi ambao unawafanya Manchester City
kuendelea kutawala katika ligi ya Epl.
Alikuwa Kelvin De Bruyne dakika ya 19 ndio alizifungua nyavu za
Arsenal baada ya kupiga shuti lililomshinda mlinga lango wa Arsenal Petr
Cech.
Goli la leo la Kelvin De Bruyne zidi ya Arsenal linamfanya kuifunga
Arsenal bao mbili na kutoa assist mbili katika michezo 5 ambayo Mbelgiji
huyo amecheza zidi ya Arsenal.
Ushindi wa leo wa City ni muendelezo wa rekodi mbovu ya Arsenal ambao
hawajawahi kushinda mchezo wowote Epl wa ugenini ambao walimaliza
kipindi cha kwanza wakiwa wamefungwa ndani ya miaka 6.
Kun Aguero aliifungia Manchester City bao la pili kwa mkwaju wa
penati bao ambalo linawafanya Arsenal kuwa timu inayoongozwa kwa
kufungwa magoli ya penati tangia kuanza kwa msimu uliopita.
Lakini Alexandre Lacazette aliyeingia akitokea benchi aliipatia
Arsenal bao la kufutia machozi dakika ya 65 na kuwafanya Arsenal kuwa
timu ambayo yenye mabao mengi kutoka kwa wachezaji wa akiba kuliko timu
yoyote Epl tangu msimu uliopita (mabao 13).
Dakika ya 74 Manchester City walifunga bao ambalo lilizua utata
kutoka kwa Gabriel Jesus baada ya kuonekana kama wachezaji wa City
walikuwa offside na mchezo kumalizika kwa City kushinda 3 kwa 1.
Mabao matatu waliyopata Manchester City hii leo yanawafanya kufikisha
idadi ya mabao 57 katika mechi zao 17 msimu huu idadi ambayo mara ya
mwisho kutokea Epl ilikuwa msimu wa mwaka 1992/1993.
No comments:
Post a Comment