Sunday, November 5, 2017

Wydad Casablanca bingwa Caf

Wydad Casablanca ya Morocco imeibuka bingwa mpya wa bara la Afrika kwa upande wa soka la vilabu baada ya kuifunga Al Ahly ya Misri bao 1-0 kwenye fainali ya pili usiku wa kuamkia leo.





Bao pekee la Wydad lilifungwa na El Karti kipindi cha pili hivyo kufanya matokeo ya jumla katika mechi zote mbili kuwa 2-1 baada ya timu hizo kutoka sare ya 1-1 wiki mbili zilizopita nchini Misri.
Ubingwa huo unakuwa wa pili kwa Wydad tangu ianzishwe ambapo mara ya kwanza kutwaa ilikuwa ni mwaka 1992. Al Ahly wao walikuwa wanatafuta ubingwa wao 9 lakini mambo yamekuwa magumu mbele ya Wydad Casablanca.



Wydad sasa itaiwakilisha Afrika kwenye michuano ya klabu bingwa ya dunia mwezi Desemba. Michuano hiyo itafanyika katika nchi za falme za kiarabu (UAE) ambapo mabingwa watetezi Real Madrid wameshafuzu kama mabingwa wa Bara la Ulaya.


No comments:

Post a Comment