Katibu
Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesisitiza kwamba wale
wachezaji wanaotanguliza fedha badala ya kupambana kwa ajili ya klabu
hawatakuwa na nafasi.
“Atakayeleta sintofahamu atachukuliwa hatua. Sisi
tunahitaji mchezaji ambaye amelenga kuisaidia klabu,” alisema.
“Kama lengo lake litakuwa ni fedha pekee na anapanga kutuvuruga basi tutaachana naye.
“Lakini
nasisitiza, tunahitaji wacheaji walio fiti ambao watakisaidia kikosi
chetu. Kama tutaona mchezaji ni majeruhi kwa muda mrefu tutaachana
naye.”
No comments:
Post a Comment