Sunday, November 5, 2017

WAKULIMA WAPATA NEEMA YA WEMA 2109

Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kushirikiana na Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB) wamekabidhi mbegu ya mahindi aina ya WEMA 2109 kwa wakulima wa wilayani Mbogwe mkoani Geita.
 
 
Mbegu hizo zimepokelewa na wakulima chini ya Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe Nsika Sizya ambaye amesema kuwa mbegu hizo zitaongeza chachu ya kilimo wilayani humo.
Changamoto kubwa waliyokuwa nayo wakulima katika Halmshauri yetu ni kukosekana kwa mbegu bora za mihogo na mahindi ila baada ya kupata mbegu hizi zitaongeza ari na chachu ya kilimo kwa wananchi”, amesema Sizya.

 

 Mbali na mbegu ya mahindi lakini pia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia imekabidhi mbegu ya mihogo aina ya Mkombozi ambayo inauwezo mkubwa wa kustahimili magonjwa ya mihogo kama batobato na michirizi ya kahawia ambayo imekuwa ikiwapatia hasara kubwa wakulima wengi na kupoteza hadi asilimia 90 za mazao.

 

 Mbegu hiyo itanufaisha wakulima wa vijiji vinne vya Mponda kilichopo Kata ya Luganga, kijiji cha Ushetu kilichopo Kata ya Ushirika, kijiji cha Lwazeze kilichopo Kata ya Ngemo na kijiji cha Iponya kilichopo Kata ya Iponya.

No comments:

Post a Comment