Saturday, November 11, 2017

ITALY WAKALIA KUTI KAVU KUELEKEA URUSI 2018

Timu ya taifa ya Ubelgiji ilikuwa uwanjani usiku wa jana kukabiliana na timu ya taifa ya Mexico ambapo katika mchezo huo Romelu Lukaku alifunga mabao mawili kati ya matatu katika suluhu ya tatu tatu.
Eden Hazard alifunga lingine huku mabao ya Mexico yakipatikana kupitia kwa Andres Guardado aliyefunga kwa penati kabla ya Hirving Lozano kuongeza mengine mawili.

Ufaransa wenyewe walikuwa uwanjani na timu yao inayosadikiwa kuwa ni kizazi cha dhahabu na kuwafunga Wales 2 kwa nunge kupitia kwa Antoine Griezman na Olivier Guroud.

Timu ya taifa ya Ureno nao bila Cr7 walicheza na Saudi Arabia ambapo Ureno waliibuka kidedea kwa mabao 3 kwa nunge mabao ya Ureno yakifungwa na Fernandes, Guedes pamoja na lile la Mario.

Katika hatua ya mtoano kuelekea kombe la dunia timu ya taifa ya Sweden iliishtua Italia baada ya kuwafunga bao 1 kwa nunge na hivyo kuwaweka Italia mashakani kulekea kombe la dunia 2018.

No comments:

Post a Comment