Taarifa zinasema Paul Pogba na Marcos Rojo wako mbioni kurejea uwanjani na mwisho wa wiki hii wanaweza kuwepo uwanjani katika kikosi cha Manchester United.
Wakati mashabiki wa United wakifurahia kupona kwa wachezaji wao sasa kuna habari mpya kwamba Phil Jones anaweza kuwa nje ya uwanja baada ya kupata majeruhi.
Jones alikuwepo wakati timu ya taifa ya Uingereza ikikipiga mechi ya kirafiki dhidi ya Ujerumani hapo jana lakini alishindwa kumaliza mchezo huo baada ya kuumia.
Taarifa zinasema Jones hakuwa fiti kuelekea mchezo wa jana, na majeruhi aliyapata dakika ya 10 lakini kocha wa timu ya Uingereza aliendelea kumchezesha hadi dakika ya 24.
Phil Jones amekuwa na msimu mzuri na anaonekana kuanza kuaminiwa na kocha Jose Mourinho kwani amekuwa akimchezesha pamoja na Chriss Smalling kama mabeki wa kati siku za usoni.
No comments:
Post a Comment