![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgVbWmaqF-lKSAVtzbD9GuVVBkMBSEv9e_m9lEdK580OWL5k4sqT0ldLW_FBj731EfNQppF4GO8_giLvHHkZyENgT6H_QKdKm9BEkOzFW7aVY4R7-ae77JcKZ32A7rEFgE8jMk9JWQGEony/s400/4606A2D600000578-5051081-image-m-8_1509860732953.jpg)
Deontay Wilder amemtwanga Bermane
Stiverne katika pambano lao la uzito wa juu na baada ya kutangazwa
mshindi, akasema waziwazi kwamba sasa anamtaka Anthony Joshua.
Wilder ameshinda katika raundi ya kwanza tu baada ya kumvurumishia mpinzani wake makonde utadhani mvua za masika.
Sasa anachotaka ni kumvaa Joshua raia wa Uingereza ili kumaliza ubishi.
Ubishi mkubwa upo kati ya Mmarekani huyo na Muingereza huyo nani ni mkali zaidi.
Lakini kipigo kikali alichotoa Wilder
kwa Stiverne kinafanya wengi waaamini atakuwa maji marefu kwa Joshua
lakini wako wanaosisitiza Joshua ni Joshua lakini lazima aimarishe
kiwango chake kwanza.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjgtDfLF8CJro-vzRwqWaaLYeQqS1T4cjl9diU6gWgiOqDZIXcx1LP_2pc3H3B3reyO2XkahEpWinIW-VSqb3m7ZII4iEvKuMlKcaDGvKJYCOimYtsa5856acj30TsiOWP56DlCzyYRw5AR/s400/4606B19600000578-5051081-image-m-18_1509861004833-1.jpg)
No comments:
Post a Comment