Kiungo Mohamed Ibrahim wa Simba, ameichezea timu yake mechi ya kirafiki iliposhinda kwa mabao 3-1 dhidi ya Rukwa FC.
Katika
mechi hiyo kwenye Uwanja wa Mandela mjini Sumbawanga, Ibrahim maarufu
kama Mo alionyesha kiwango kizuri kama ilivyokuwa kwa wachezaji wengi
waliopata nafasi.
Lakini kabla ya mechi hiyo, Mo alionekana kama ni mtu asiye na furaha.
Hata wakati Kocha Joseph Omoga akizungumza na wachezaji wote baada ya mazoezi, Mo alionekana kama si mtu mwenye furaha sana.
Hata
kama atakuwa haonyeshi, lakini inaonekana Mo amekuwa hafurahii kukaa
benchi jambo ambalo limekuwa likihusishw akwamba anaweza kwenda Yanga.
Hata
hivyo, wakati akicheza mechi alionekana ni mwenye furaha na aliyetaka
kufanya vizuri ingawa hiyo bado haifuti kwamba hawezi kuwa na furaha
akiendelea kukaa benchi.
Kabla,
Mo alishauriwa kuendelea kujituma na kutafuta nafasi lakini wakamshauri
kuondoka ili apate nafasi zaidi ya kucheza akiwa sehemu nyingi.
Hata
hivyo, Mo bado hajafungua mdomo kulizungumzia hilo na hasa suala la
kuona kama anaweza kwenda Yanga ambako atapata nafasi zaidi ya kucheza.
No comments:
Post a Comment