Kocha Joseph Omog leo ataingoza Simba mechi yake ya tisa ya Ligi Kuu
Bara msimu huu, mechi hiyo itakuwa ugenini kwenye Uwanja wa Sokoine
mjini Mbeya.
Simba inaivaa Mbeya City na mwendo wa Simba umekuwa ni kushinda moja, inayofuatia ni sare.
Ushindi halafu sare imekuwa ni kawaida kwa Simba kwa kuwa imeshinda mechi nne na kutoka sare nne.
Mechi ya tisa ni leo, maana yake kama mwendo ni huo, Simba itashinda na inayofuata ni dhidi ya Prisons, itakuwa sare tena?
Lakini Mbeya City nao wanaweza
kujiuliza na kukataa kuwa daraja la Simba kwenda na mwendo wake wa
ushindi, sare, ushindi halafu sare tena.
Kama ikiwa hivyo, itakuwaje kwa Omog
ambaye inaonekana wazi, mechi mbili za Mbeya, akianza na ya leo dhidi
ya Mbeya City na ile itakayofuata dhidi ya Prisons, zitakuwa ni mtihani
kwake.
Kama akishinda zote, atakuwa na
nafasi ya kubaki Simba lakini ikiwa ushindi na sare atajichongea na
akipoteza zote basi, hakuna ubishi tena, safari itakuwa imemkuta.
No comments:
Post a Comment