Saturday, November 11, 2017

Jamhuri Kihwelo lazima nisajili

Itakapofika Novemba 15, mwaka huu ndipo dirisha dogo la usajili ndipo litakapofunguliwa, sasa Kocha wa Dodoma FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ Amesema ni lazima asajili wachezaji wa kumfanyia kazi kwani waliopo hawatoshi.

Kwenye Kundi C la Ligi Daraja la Kwanza, Dodoma FC ipo kileleni na pointi 18 huku wakitakiwa kushinda mechi tano ili kujihakikishia kupanda Ligi Kuu Bara msimu ujao.

Julio amesema; “Lazima niongeze wachezaji wengine kwani kati ya wachezaji nilionao natakiwa kuwaongezea nguvu ili tupande ligi kuu.”

No comments:

Post a Comment