Kapteni
wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, amewapoza mashabiki wa timu yake
kwa kuwaambia watulie kwani wao wachezaji wamejipanga kutwaa ubingwa wa
Kombe la Mapinduzi mwaka huu.
Cannavaro
ametoa kauli hiyo wakati mashabiki wa Yanga wakiwa na kumbukumbu ya
kufungwa mabao 2-0 na Mbao FC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa
wikiendi iliyopita.
Beki huyo hakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga ambacho kilifungwa na Mbao kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Cannavaro
aliyedumu kikosini hapo kwa zaidi ya miaka kumi, amesema kuwa wamepanga
kuwafuta machozi Wanayanga kwa kutwaa Kombe la Mapinduzi.
“Najua
kwamba mashabiki wetu wana hasira na sisi baada ya kile kipigo
tulichokipata kutoka kwa Mbao, lakini nawaambia tutawafuta machozi kwa
kuchukua ubingwa wa Mapinduzi msimu huu.
“Tumejipanga
na tumedhamiria kuchukua ubingwa huu na hilo linawezekana, pia
tutatumia michuano hii kama sehemu ya kujiandaa na ligi pamoja na
michuano ya kimataifa,” alisema Cannavaro.
Yanga
kwa sasa wanafundishwa na makocha wasaidizi, Noel Mwandila na Shadrack
Nsajigwa ambao walianza kampeni yao ya Kombe la Mapinduzi Jumanne hii
kwa kuifunga Mlandege mabao 2-1 katika Kundi B.
Halafu juzi usiku ikaifunga JKU bao 1-0 na jana usiku ilicheza na Taifa Jang’ombe.
No comments:
Post a Comment