![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiB8ihUeMyvWm7n1NiqZW_TWHhHfbIgf6XLaQtulbgbwkNtH6375VDey7drYEbkzoP2A9NAymabeyMuPXdRc-HDSNm2fjtd4h7Fjd8CHqQG75e6gMTCJIxRLA1vZKF_lskerU4WjRxcJ4E/s400/CIOABA-KOCHA-AZAM-1_1508431648-1600x705.jpg)
Bosi
wa benchi la ufundi la Azam FC, Aristica Cioaba, raia wa Romania na
wasaidizi wake, wanakoshwa na soka la mshambuliaji wao mpya, Bernard
Arthur raia wa Ghana ambaye amekuwa msaada mkubwa katika ushambuliaji.
Arthur
amejiunga na Azam akitokea Liberty Professional ya kwao Ghana, Jumatano
wiki hii aliiongoza timu hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya
Jamhuri kwenye Kombe la Mapinduzi.
Katika
ushindi huo, Arthur alifunga bao moja kati ya matatu waliyopata na
kuiwezesha Azam kufikisha pointi sita kabla ya mchezo wa jana dhidi ya
URA na leo dhidi ya Simba.
Cioaba alisema Arthur amekuwa msaada katika safu yao ya ushambuliaji ambayo ilikuwa inafunga mabao machache.
“Amekuja
vizuri kwa kuingia ndani ya timu na kutupa matokeo yale ambayo tulikuwa
tunayataka sisi, utaona kwamba ana muendelezo mzuri wa kufunga tangu
alipoanza kutufungia dhidi ya Stand United katika ligi kuu.
“Naamini
kwa uwezo wake kuna kitu kikubwa ambacho atakifanya kwenye mechi
zinazokuja, kwa sasa naamini mshambuliaji huyu ni mtu sahihi kabisa
katika kikosi chetu ukizingatia mwenzake, Mbaraka Yusuph yuko nje
kutokana na majeraha,” alisema kocha huyo.
No comments:
Post a Comment