NAHODHA
wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ameanza mazoezi mepesi chini ya
uangalizi wa Daktari baada ya kupona maumivu ya goti yaliyomuweka nje
kwa miezi miwili.
Mshambuliaji huyo wa KRC Genk ya
Ubelgiji amesema kwa sasa anafanya mazoezi maalum ya kukimbia, kuchezea
mpira na ya viungo chini ya uangalizi wa daktari, ikiwa ni hatua ya
mwisho kuelekea kurejea uwanjani.
“Nipo
kwenye mazoezi ya mwisho, hatua ya mwisho kabla sijajiunga na timu,
nafanya mazoezi chini ya usimamizi wa mtaalamu (Daktari) wa maozezi ya
viungo,”amesema Samatta.
Samatta
amekamilisha wiki sita za mapumziko kufuatia kuumia mishipa midogo ya
goti lake la mguu wa kulia ambayo ilichanika Novemba 4, mwaka jana
akiichezea KRC Genk ikilazimishwa sare ya 0-0 na Lokeren katika mchezo
wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk.
Samatta
aliumia akiichezea mechi ya 70 Genk tangu alipojiunga nayo Januari
mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
(DRC). Na katika mechi hizo 70, Samatta, mshambuliaji wa zamani wa
Mbagala Market, African Lyon na Simba za Tanzania, amefunga mabao 22
kwenye mashindano yote
No comments:
Post a Comment