![](https://www.eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/news/2018/01/05/YANGA%20AJIBU.jpg?itok=cuxRrKJX×tamp=1515168906)
atibu mkuu wa timu hiyo Charles Mkwasa amesema usaili huo utafanyika Jumapili hii Januari 7 mwaka huu, kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.
''Tunawaomba wazazi wenye watoto chini ya umri wa miaka 15 kuwaleta watoto wao kwenye usaili wa kusaka vijana wenye vipaji vya kucheza soka ili wafanyiwe usaili na waweze kusajiliwa na klabu ya Yanga'', amesema Mkwasa.
Aidha Mkwasa amesema usaili huo utaendeshwa na wakongwe waliowahi kuichezea Yanga, Kama Keneth Mkapa, Maalim Saleh, Edibily Lunyamila na Ramadhani Kampila.
![](https://www.eatv.tv/sites/default/files/inline/images/YANGA%204444.jpg)
Yanga inaboresha kikosi chake cha vijana ambacho kimekuwa hakifanyi vizuri ukilinganisha na timu zingine za vijana kama za Azam FC pamoja na timu ya vijana ya Simba ambayo iliibuka bingwa wa ligi ya vijana msimu uliopita.
No comments:
Post a Comment