Wednesday, January 10, 2018

Usajili wa Coutinho waiumiza United


Ni mwendo wa pesa tu barani Ulaya, na kwa sasa kila mchezaji maarufu ukimgusa lazima uwe na kuanzia £70m na ndio maana haikushangaza sana kwa Philippe Coutinho kwenda Barcelona kwa dau la £145m.

Lakini usajili huu umeanza kuongeza thamani ya wachezaji wengine na vilabu vingine vimeamua kuongeza dau kwa wachezaji wao baada ya kuonekana kwamba lolote linawezekana katika biashara ya sasa ya soka.
Moja kati ya vilabu ambavyo inatajwa kuongeza bei ya mchezaji wake ni klabu ya Juventus, ripoti kutoka nchini Italia zinasema kwa sasa Juventus wameamua kwamba kwa timu yoyote inayomtaka Paulo Dyabala lazima ije na £150m.
Pamoja na taarifa kutoka kwa mkurugenzi wa Juventus Giussepe Marotta kwamba Juventus haiwezi kumuuza Dyabala kwa kiasi chochote kile cha pesa lakini jarida moja la michezo nchini Italia limefahamu kuhusu mauzo ya Dyabala.
Manchester United wanaonekana mstari wa mbele kumnunua Dyabala ambapo hapo mwanzo alitajwa kuwa na thamani ya £80m lakini sasa itawalazimu United kutoa kiasi mara mbili ya ambacho wangetoa mwanzo.

No comments:

Post a Comment