![](https://globalpublishers.co.tz/wp-content/uploads/2017/12/CHIRWA-2.jpg)
Ikiwa ndiyo siku ya kwanza
anaichezea Yanga katika michuano ya Kombe la Mapinduzi, mshambuliaji
Obrey Chirwa amekosa penalti ya mwisho na kuing’oa Yanga katika michuano
ya Mapinduzi.
URA ya Uganda imeitoa
Yanga kwa mikwaju 5-4 na kufanikiwa kutinga fainali ya Kombe la
Mapunduzi. Mwaka 2016, URA iliing’oa tena Yanga katika hatua hiyo kwa
mikwaju ya penalti.
Chirwa alikuwa amegoma
kujiunga na Yanga akitaka alipwe fedha zake za usajili. Lakini leo
ameungana na kikosi hicho akitokea Dar es Salaam. Ikiwa ndiyo siku ya
kwanza amejiunga na Yanga, Chirwa alitokea benchi kuchukua nafasi ya
Pius Buswita na dakika 90 zikaisha kwa sare ya bila mabao, ikaingia
mikwaju ya penalti.
Chirwa ndiye alikuwa wa mwisho upande wa Yanga baada ya Papy Tshishimbi, Hassan Kessy, Raphael Daud na Gadiel Michael kupata.
No comments:
Post a Comment