![](https://www.eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/news/2018/01/05/BANDA%20JR%202.jpg?itok=0WRdhT7a×tamp=1515159020)
Banda amesema atafanya hivyo kwasababu anatambua kuwa wapo vijana wengi ambao wana ndoto za kufika mbali zaidi kisoka, hivyo wanahitaji msaada kutoka kwa watu ambao wapo mbele katika soka.
''Unapocheza nje ya Tanzania ni vizuri kuonyesha mchango wako kwa vijana walio chini yako, kwahiyo hilo ndio lengo langu na sitaishia tu kujenga kituo nitaendelea kutoa vifaa vya michezo kwaajili ya vijana wenye ndoto za kuwa wachezaji wakubwa'', ameongeza.
![](https://www.eatv.tv/sites/default/files/inline/images/BANDA%20JR.jpg)
Banda alisajiliwa na Baroka FC kwenye usajili wa kiangazi Juni 2017, baada ya kuonesha kiwango kizuri alipokuwa nchini Afrika Kusini na kikosi cha Taifa Stars kwenye michuano ya COSAFA 2017. Baroka inashika nafasi ya nne kwenye ligi kuu ya humo ikiwa na alama 22 baada ya michezo15
No comments:
Post a Comment