![](https://globalpublishers.co.tz/wp-content/uploads/2016/04/453788718.jpg)
Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho.
KOCHA wa Manchester United, Jose Mourinho amethibitsha kwa ujanja kuwa naye anamtaka Alexis Sanchez baada ya kumpa sifa nyingi.Mourinho alisema ni vigumu kwa klabu yoyote kuacha fursa ya kusajili nyota mwenye kipaji aina ya Sanchez akitokea yupo soko.
![](https://globalpublishers.co.tz/wp-content/uploads/2018/01/sanchez.jpg)
Alexis Sanchez.
“Klabu yoyote makini iwe kama ni Januari, Februari au Julai ikitokea
kuna staa yupo sokoni lazima itamchangamkia ingawa sina maana ya
Sanchez,” aliongea kijanja Mourinho.Mourinho alidai hataki kuongelea zaidi kuhusu Sanchez ingawa anamkubali kama mchezaji mzuri mwenye kipaji cha hali ya juu.
Manchester City na Manchester United ziko kwenye vita kali ya kumwania Sanchez, ambaye mkataba wake na Arsenal unamalizika mwishoni mwa msimu huu.
Manchester United inadaiwa imetenga dau la kiasi cha pauni milioni 35 na iko tayari kumpa mshahara wa pauni 250,000 kwa wiki.
No comments:
Post a Comment