Kampuni inayokusanya taarifa za takwimu mbali mbali za michezo
iitwayo CIES Football Obsevatory imetoka na taarifa mpya kuhusu kiwango
cha wachezaji wenye uwezo mkubwa kwa kukokota mipira(dribles).
TIMU
za Tanzania Prisons na Stand United zimekamilisha idadi ya timu nane za
kucheza hatua Robo Fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup
(ASFC) baada ya ushindi kwenye mechi zao za jana.
SIMBA
SC imezidi kuukimbilia kwa kasi ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara baada ya ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Mbao FC ya Mwanza jioni ya jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mshambuliaji
Mganda, Emmanuel Okwi alifunga mabao mawili moja kila kwa kipindi kabla
ya kuumia na kutolewa wakati mabao mengine yalifungwa na Shiza Kichuya,
Erasto Nyoni na Mghana, Nicholaus Gyan. Ushindi
huo unaifanya Simba itimize pointi 45 baada ya kucheza mechi 19,
ikiendelea kukaa kileleni mwa Ligi Kuu, ikifuatiwa na mabingwa watetezi,
Yanga wenye pointi 37 za mechi 18, wakati Mbao FC inabaki nafasi ya 10
kwa pointi zake 19 za mechi 19. li
kuanza kupata mabao, benchi la Ufundi la Simba chini ya kocha Mfaransa,
Pierre Lechantre anayesaidiwa na Mrundi, Masoud Juma lililazimika
kufanya mabadiliko ya mapema kipindi cha kwanza katika safu ya kiungo
kwa kumtoa Said Hamisi Ndemla na kumuingiza Muzamil Yassin baada ya nusu
saa. Mabadiliko
hayo yalibadilisha kabisa mwelekeo wa mechi, kutoka Mbao FC kutawala
hadi Simba SC ambayo wiki ijayo itamenyana na El Masry ya Misri katika
Raundi ya Kwanza ya kombe la Shirikisho Afrika kuuteka mchezo. Shiza
Ramadhani Kichuya akafungua sherehe za mabao za Simba kwa kufunga bao
la kwanza dakika ya 38 akimalizia pasi ya mtokea benchi, Muzamil. Mganda
Emmanuel Okwi akaifungia Simba SC bao la pili dakika ya 40 kwa penalti,
baada ya yeye mwenyewe kuanguka kwenye boksi wakati anadhibitiwa na
beki wa Mbao, David Mwasa. Refa
Erick Onoka kutoka Arusha akawanyima Simba SC penalti sahihi zaidi ya
aliyowapa mwanzo baada ya Okwi kuangushwa kwenye boksi na Nahodha wa
Mbao FC, Mrundi, Yusuph Ndikumana ambaye leo alicheza chini ya kiwango. Kipindi
cha pili, Mbao FC wanaofundishwa na kocha Mrundi, Etienne Ndayiragijje
walikianza vizuri wakishambulia kujaribu kutafuta mabao ya kusawazisha,
lakini safu ya ulinzi ya Simba chini ya kipa Aishi Salum Manula
ilisimama imara. Kibao
kikaigeukia Mbao FC na wakajikuta wanapachikwa mabao matatu ndani ya
dakika 20, Okwi akianza kufunga dakika ya 69 kwa shuti la mguu wa kulia
baada ya kupokea pasi ya Muzamil Yassin. Okwi
anatolewa nje anachechemea baada ya kuumia kufuatia kugongana na beki
wa Mbao FC, Amos Charles kwenye boksi na nafasi yake kuchukuliwa na
Mrundi, Laudit Mavugo. Beki
mkongwe anayeweza kucheza kama kiungo pia, Erasto Edward Nyoni
akaifungia Simba SC bao la nne dakika ya 82 kwa shuti la mpira wa adhabu
kutoka umbali wa mita 19 kasoro kidogo, baada ya Muzamil kuangushwa. Refa
Onoka akamtoa nje kwa nyekundu Nahodha wa Mbao FC, Ndikumana dakika ya
84 baada ya kumuonyesha kadi ya pili ya njano kufuatia kumchezea rafu
Mavugo Mrundi mwenzake, Mavugo. Nicholaus
Gyan akaifungia Simba SC bao la tano dakika ya 86 kufuatia krosi ya
beki wa kulia, Shomary Kapombe kuzua kizaazaa langoni kwa Mbao FC. Kikosi
cha Simba SC; Aishi Manula, Shomari Kapombe, James Kotei, Yussuph
Mlipili, Erasto Nyoni, Asante Kwasi, Jonas Mkude, Said Ndemla, Shiza
Kichuya/Rashid Juma dk86, Nicholas Gyan na Emmanuel Okwi/Laudit Mavugo
dk80. Mbao
FC; Iyvan Rugumandiye, Boniphace Maganga, Amos Charles, David Mwasa,
Yusuph Ndikumana, Ibrahim Njohole/ Said K. Said dk57, Herbet Lukindo,
George Sangija, Habibu Hajji, James Msuva/Rajesh Kotecha dk51 na
Emmanuel Mvuyekure/Ismail Ally dk70.
MCHEZO
wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya wenyeji Mtibwa Sugar na
Yanga SC ya Dar es Salaam uliopangwa kufanyika Machi 3, mwaka huu Uwanja
wa Jamhuri mjini Morogoro umeahirishwa. Sababu
za kuuahirisha mchezo huo namba 170 ni kuipa Yanga nafasi nzuri ya
maandalizi ya mchezo wake wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township
Rollers ya Botswana Machi 6 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Busara
za Bodi chini ya Mwenyekiti wake, Clement Sanga ambaye pia ni Kaimu
Mwenyekiti wa Yanga SC zimeielekeza kuusogeza mbele mchezo wa Ligi Kuu
ili kuwapa wawakilishi hao wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa fursa
nzuri ya maandalizi.
Baada
ya kukata tiketi ya Robo Fainali ya michuano ya Azam Sports Federation
Cup (ASFC) kufuatia ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Maji Maji Uwanja wa
Maji Maji mjini Songea Jumapili, Yanga iliondoka mjini humo mapema
Jumatatu kwa basi lake kwenda Mtwara tayari kwa mchezo mwingine wa Ligi
Kuu dhidi ya wenyeji, Ndanda FC Jumatano Uwanja wa Nangwanda Sijaona. Mabao
ya Yanga Jumapili yalifungwa na kiungo Pius Charles Buswita kwa kichwa
dakika ya 40 akimalizia krosi ya beki Mwinyi Hajji Mngwali kutoka upande
wa kushoto baada ya kuanzishiwa kona fupi na kiungo mwenzake,
waliyekuwa wakicheza naye pale mbele, Ibrahim Ajib na winga Emmanuel
Martin dakika ya 57 akimalizia kwa kichwa krosi ya beki wa kulia, Hassan
Kessy aliyemlamba chenga Mpoki Mwakinyuki. Bao
pekee la Maji Maji lilifungwa na kiungo Jaffar Mohammed kwa kichwa
dakika ya 61, akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na beki Aziz Sibo
kufuatia Nahodha, Kevin Yondan kumchezea rafu Marcel Boniventura. Yanga
ilikata tiketi ya kwenda Raundi ya Kwanza ya michuano ya Ligi ya
Mabingwa Afrika Jumatano iliyopita licha ya sare ya 1-1 na wenyeji,
Saint Louis Suns United katika mchezo wa marudiano wa Raundi ya Awali
Uwanja wa Linite. Mabingwa
hao wa Tanzania wamesonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 2-1 baada ya
Februari 10 kushinda 1-0 pia Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, bao pekee
la kiungo Juma Mahadhi aliyekosekana uwanjani kwenye mechi ya marudiano
kwa sababu ya homa. Kwa
kuitoa St Louis, Yanga itakutana na Township Rollers ya Botswana katika
Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ambayo nayo iliitoa El
Merreikh ya Sudan, mechi ya kwanza ikichezwa Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam Machi 6 kabla ya kwenda Gaborone kwa mchezo wa marudiano, Machi
17.
Cristiano
Ronaldo (kulia) akishangilia na wenzake kumpongeza Marcelo baada ya
kuifungia Real Madrid bao la tatu dakika ya 84 katika ushindi wa 4-1
dhidi ya wenyeji, Valencia kwenye mchezo wa La Liga leo Uwanja wa
Mestalla. Ronaldo naye alifunga mabao mawili, yote kwa penalti dakika
za 16 na 38 wakati bao la nne limefungwa na Toni Kroos dakika ya 89,
huku la Valencia likifungwa na Santi Mina dakika ya 58
WENYEJI,
Morocco na Sudan wamefanikiwa kwenda Nusu Fainali za michuano ya
Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) baada ya ushindi dhidi ya Namibia na
Zambia usiku wa jana.
KIUNGO wa Simba, Said Ndemla, sasa anajiandaa kusaini mkataba mpya wa
kuendelea kuwepo Msimbazi huku ikielezwa lile dili la kwenda kucheza
Ulaya limeyeyuka.
Ndemla ambaye mkataba wake wa sasa na Simba unamalizika Aprili, mwaka
huu, mwishoni mwa mwaka jana alikwenda Sweden kufanya majaribio kwenye
timu ya AFC Eskelistuna na kufuzu.
Hata hivyo, licha ya kufuzu majaribio hayo, Ndemla ameshindwa kujiunga na timu hiyo.
Taarifa kutoka ndani ya Simba zinasema kuwa, uongozi umeridhishwa na
kiwango cha Ndemla, hivyo wameona bora waendelee kuwa naye ili
kukiongezea nguvu kikosi katika mechi za Kombe la Shirikisho Afrika.
“Mkataba wake unaelekea ukingoni lakini wakati wowote anaweza
kuongezewa kwa sababu uongozi unaridhishwa na kiwango chake ukizingatia
kwamba tuna michuano ya kimataifa.
“Hii inamaanisha kuwa, huu si wakati wa kuacha wachezaji kama yeye,” kilisema chanzo hicho.
Alipotafutwa meneja wa mchezaji huyo, Jamal Kisongo kuzungumzia
mustakabali wa Ndemla, alisema: “Lile dili lake kule Sweden tumewaachia
Simba waamue kwani bado ni mchezaji wao, vyovyote watakavyosema ni sawa
hakuna shida.”
Wakati hayo yakijiri, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba,
Zacharia Hans Poppe amemuahidi kiungo huyo kumpatia gari kutokana na
kiwango chake bora alichokionyesha msimu huu
Straika Pierre-Emerick Aubameyang kutoka Borussia Dortmund ya Ujerumani.
LONDON, England
ARSENAL chini ya kocha wake Arsene Wenger inapambana kuhakikisha
inamsajili straika Pierre-Emerick Aubameyang kutoka Borussia Dortmund ya
Ujerumani.
Aubameyang raia wa Gabon anatakiwa na Arsenal kwa udi na uvumba ili
kuziba nafasi ya straika Alexis Sanchez ambaye anatarajiwa kujiunga na
Manchester United au Manchester City.
Maisha ya Aubameyang katika Klabu ya Borussia Dortmund sasa siyo
mazuri na inaonekana wazi straika huyo anataka kuondoka na klabu
iliyoonyesha nia ya kumsajili ni Arsenal.
Wenger hana jinsi zaidi ya kumuachia Sanchez kwenda jijini Manchester
kwani isipofanya hivyo sasa, inaweza kumtoa bure katika usajili ujao
kabla ya msimu mpya.
Hata hivyo zipo sababu zinazoonyesha kuwa, Aubameyang anaweza kuisumbua Arsenal kutokana na sababu zifuatazo:
#5 Kulazimisha ushindi
Aubameyang anajua kufunga na akiwa karibu na lango ni mtu hatari sana
kwa wapinzani. Hata hivyo, ana tatizo la kutokuwa mpambanaji kwa ajili
ya timu na hana njia nyingi za kuwabuguzi mabeki, akishindwa njia moja
ndiyo basi tena. Anategemea kufunga kwa kutengenezewa nafasi na
wakishindwa kumfanyia hivyo ndiyo basi tena.
#4 Tatizo la ulinzi
Moja kati ya matatizo makubwa ya Aubameyang awapo uwanjani ni mchango
wake wa kukaba. Kwa soka la sasa hasa England, kukaba ni kazi ya
mshambuliaji pia ili kupunguza kasi ya adui. Sasa Aubameyang yeye si
mzuri katika kukaba hivyo atapata tabu katika mfumo huo.
#3 Hayupo kama zamani
Aubameyang wa sasa si yule wa msimu mmoja au miwili nyuma, ameshuka
pia vituko vyake nje ya uwanja ni tatizo kichwani mwake. Sawa, sasa
anaweza kuwa amefunga mabao 21 katika mechi 23 msimu huu, lakini
hailingani na nafasi anazopoteza uwanjani sasa katika kikosi cha
Borussia Dortmund.
#2 Gharama yake haiendani na umri
Aubameyang sasa ana umri wa miaka 28, hivyo dau la Borussia Dortmund
la kumuuza kwa pauni milioni 53 (Sh bilioni 162.8), haiwezi kuwa na
faida kwao kwani hatoweza kucheza kwa ushindani kwa muda mrefu. Hii ina
maana kuwa, Arsenal haitaweza kumtumia kwa muda mrefu.
#1 Hawezi kuwa Alexis Sanchez
Ukweli ni kwamba, Aubameyang hawezi kuwa mbadala sahihi wa Alexis
Sanchez. Arsenal inadhani Aubameyang ndiye mbadala sahihi wa Sanchez
lakini ukweli ni kwamba wawili hao wapo tofauti kabisa. Aubameyang
anacheza kwa mtindo mmoja na kwa kutumia upande mmoja tu lakini Sanchez
yupo pande zote. Hapa ndipo Arsenal inapoongeza nguvu pia kumnasa Malcom
wa Bordeaux.
Baada ya mgomo wa muda wa takribani wiki mbili, kipa Beno Kakolanya hatimaye amerejea mazoezini Yanga.
Kakolanya
amerejea na kuendelea na mazoezi na wenzake kwenye Uwanja wa Uhuru
jijini Dar es Salaam kuendelea kujiandaa na mechi zijazo za Ligi Kuu
Bara.
Kipa huyo mzoefu aliyejiunga na Yanga akitokea Prisons ya Mbeya, aliweka mgomo akitaka kumaliziwa fedha alizokuwa anadai.
Hata
hivyo, ilionekana uongozi wa Yanga ulikuwa ukipambana kumrejesha Obrey
Chirwa ambaye pia aligomea kwao Zambia kutokana na kutolipwa fedha zake
pia.
Baadaye,
uongozi huo ulifanikiwa kumrekesha Chirwa timu ikiwa kwenye michuano ya
Kombe la Mapinduzi na sasa Kakolanya naye amerejea.
Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma bado ni majeruhi na hajajiunga na wenzake.
Lakini
jana aliamua kuwatembelea wenzake mazoezini kwenye Uwanja wa Uhuru
wakati wakiendelea kujifua kujiandaa na mechi za Ligi Kuu Bara.
Raia
huyo wa Zimbabwe, ameendelea kukaa nje kwa zaidi ya miezi miwili sasa
na imekuwa zaidi ya wiki tatu tokea arejee Dar es Salaam akitokea kwao
Zimbabwe ambako ilielezwa amekwenda kupata matibabu nchini Afrika
Kusini.
Beki
kisiki wa kati wa Yanga, Kelvin Yondani anatarajiwa kuikosa mechi ya
kesho dhidi ya ya Ligi Kuu Bara itakayochezwa kwenye
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Yondani ataikosa mechi hiyo kutokana na kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano alizozipata kwenye mechi zilizopita za ligi kuu.
Kutokana
na hali hiyo, timu inaweza kumtumia beki wa kati Nadir Haroub
‘Cannavaro’ au Said Makapu kucheza nafasi hiyo ya beki ya kati pamoja na
Vicent Andrew ‘Dante’.
Taarifa
zinaeleza Benchi la Ufundi la Yanga tayari limeanza kuchukua tahadhari
ya kuwaandaa baadhi ya wachezaji akiwemo Cannavaro atakayecheza nafasi
ya Yondani.
“Yondani
ameondolewa kwenye mipango ya kocha katika kuelekea mechi dhidi ya Ruvu
itakayochezwa Jumapili Uwanja wa Taifa.
“Beki
huyo ataukosa mchezo huo kutokana na kutumikia adhabu ya kadi tatu za
njano alizozipata katika michezo iliyopita ya ligi kuu,” alisema mtoa
taarifa huyo.
Meneja
Mkuu wa Yanga, Hafidh Saleh alithibitisha Yondani kuondolewa kikosini;
“Ni kweli Yondani hatakuwepo katika mechi dhidi ya Ruvu kwani ana adhabu
ya kadi tatu za njano.”
WAZIRI
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe leo
amewatembelea wachezaji wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa
miaka 17, Serengeti Boys waliopo kambini kwenye hostel za Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF), zilizopo Uwanja wa Karume, Dar es Salaam. Katika
ziara yake hiyo, Waziri Mwakyembe alijionea namna wachezaji hao
wanaoshi na kufanya mazoezi chini ya walimu wao, Mdenmark Kim Poulsen na
Msaidizi wake, Oscar Milambo. Pamoja
na kuzungumza nao na kuwatia moyo ili wajitume zaidi, Waziri Mwakyembe
aliwaachia ujumbe wa Serikali wachezaji wa Serengeti Boys ambao wote
hawazidi umri wa miaka 16. Dk.
Mwakyembe akitoa salamu za Serikali amewaambia vijana wanaounda timu
hiyo kuwa serikali yao inawaamini na wanalo jukumu la kuiperusha vyema
bendera ya Tanzania. Amewataka
kupambana kwaajili ya Tanzania na kuhakikisha wanafanya vyema kwenye
kila mashindano huku akiwataka makocha wa kikosi hicho kuwapa mafunzo
mazuri kwa ustawi wa Vijana hao. Aidha,
Dk. Mwakyembe amesema anaamini Vijana hao watakuwa bora chini ya TFF
iliyopo madarakani inayoongozwa na Rais Ndugu Wallace Karia. "Naamini mtaimarika na kuwa bora maana hata TFF hii sasa ina ari na morali kubwa" amesema Dk. Mwakyembe. Katika
ziara yake hiyo Dk. Mwakyembe alipata nafasi ya kutazama Serengeti Boys
ikiifunga 4-1 Makongo Sekondari katika mchezo wa kirafiki. Kabla
ya mchezo huo Serengeti Boys walicheza mchezo mwingine wa kirafiki
dhidi ya Kituo cha Bombom na kutoa sare ya kufungana bao 1-1. Wachezaji
34 wakiwemo 30 wa ndani na makipa wane, wapo kambini Serengeti Boys
tangu mwanzoni mwa mwezi hadi Januari 28, 2018 kwa maandalizi ya
michuano CECAFA Challenge U-17. Maandalizi
hayo ya Serengeti Boys yatakwenda sambamba na kucheza mechi za kirafiki
kabla ya kuhairisha kambi hiyo itakayokuwa ikifanyika mara kwa mara na
mpango uliopo ni kila mwezi timu hiyo kuingia kambini.
Azam Fc imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi, hiyo ni baada ya kuifunga URA ya Uganda kwa penati 4-3.
Awali katika dakika 90 za mchezo huo, timu hizozilitoka suluhu ya 0-0
katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Amaan, jana usiku kisiwani
Unguja.
Baada ya kukabidhiwa ubingwa huo, taarifa kutoka Azam FC zinaeleza
kuwa ubingwa huo wameutoa zawadi kwa kiungo wa timu hiyo, Salum Abubakar
‘Sure Boy’, na hii ni baada ya kufiwa na Mama yake mzazi wiki iliyopita
wakati akiwa na timu hiyo kwenye harakati za kuwania taji hilo.
Hadi Azam FC inatwaa ubingwa, imeweza kucheza jumla ya mechi sita,
ikishinda mara tano na kupoteza mmoja huku ikiruhusu nyavu zake kuguswa
mara moja tu, na hii ni walipofungwa bao 1-0 dhidi ya URA kabla ya
kulipa kisasi kwenye mchezo huo wa fainali.
Kikosi hicho kilitarajiwa kuondoka visiwani Zanzibar, asubuhi ya leo
Jumapili kurejea jijini Dar es Salaam tayari kabisa kuanza maandalizi ya
kuwakabili Majimaji ya Songea na Tanzania Prisons ya Mbeya, katika
mechi zijazo mbili za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL)
zitakazofanyika wiki ijayo.
KOCHA wa Manchester United, Jose Mourinho amethibitsha kwa ujanja kuwa naye anamtaka Alexis Sanchez baada ya kumpa sifa nyingi.
Mourinho alisema ni vigumu kwa klabu yoyote kuacha fursa ya kusajili nyota mwenye kipaji aina ya Sanchez akitokea yupo soko.
Alexis Sanchez.
“Klabu yoyote makini iwe kama ni Januari, Februari au Julai ikitokea
kuna staa yupo sokoni lazima itamchangamkia ingawa sina maana ya
Sanchez,” aliongea kijanja Mourinho.
Mourinho alidai hataki kuongelea zaidi kuhusu Sanchez ingawa anamkubali kama mchezaji mzuri mwenye kipaji cha hali ya juu.
Manchester City na Manchester United ziko kwenye vita kali ya
kumwania Sanchez, ambaye mkataba wake na Arsenal unamalizika mwishoni
mwa msimu huu.
Manchester United inadaiwa imetenga dau la kiasi cha pauni milioni 35 na iko tayari kumpa mshahara wa pauni 250,000 kwa wiki.
Mapya yameibuka baada ya moja kati ya matajiri wa klabu ya Everton
Farhadi Moshri kuibuka na kutaja masuala ya ushirikina kuwa kati ya
mambo ambayo yalimfanya Lukaku kuondoka katika klabu yao.
Ni mwendo wa pesa tu barani Ulaya, na kwa sasa kila mchezaji maarufu
ukimgusa lazima uwe na kuanzia £70m na ndio maana haikushangaza sana kwa
Philippe Coutinho kwenda Barcelona kwa dau la £145m.
Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Ismail Aden Rage,
ameibuka na kusema kuwa, ndani ya klabu hiyo kuna tatizo na kama
hawatakuwa makini, basi kuna uwezekano hata ubingwa wa Ligi Kuu Bara
msimu huu timu hiyo ikauokosa.
BENCHI la ufundi la Simba chini ya
kaimu kocha wake mkuu, Masoud Djuma, raia wa Burundi, limempa tahadhari
beki mpya wa timu hiyo, Asante Kwasi, raia wa Ghana,
Ikiwa ndiyo siku ya kwanza
anaichezea Yanga katika michuano ya Kombe la Mapinduzi, mshambuliaji
Obrey Chirwa amekosa penalti ya mwisho na kuing’oa Yanga katika michuano
ya Mapinduzi.
RAIS
wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia ametuma salamu za
rambirambi kufuatia kifo cha beki wa zamani wa kimataifa wa Tanzania,
Omary Kapera aliyefariki dunia juzi kuzikwa jana mchana.
MZAMBIA wa Yanga, Obrey Chirwa, amerejea nchini juzi Ijumaa usiku
akitokea kwao, huku uongozi ukisisitiza kwamba kuna ishu wanaweka sawa
kabla hajajiunga na wenzie Zanzibar.
EMMANUEL Okwi amewaambia mashabiki wa Simba kwamba licha ya yeye
kutokuwa sehemu ya kikosi kwa sasa katika michuano ya Mapinduzi lakini
kwa jinsi alivyoona kwenye Azam TV hakuna ya kuwazuia kubeba ndoo.
NAHODHA
wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ameanza mazoezi mepesi chini ya
uangalizi wa Daktari baada ya kupona maumivu ya goti yaliyomuweka nje
kwa miezi miwili.
Jose Mourinho na Antonio Conte kwa muda sasa wamekuwa wakitupiana
maneno ya chinichini katika mikutano na waandishi wa habari japo chanzo
haswa cha wawili hao kurushiana vijembe hakifahamiki.
Beki wa Tanzania anayekipiga kwenye klabu ya Baroka FC inayoshiriki ligi
kuu ya soka nchini Afrika Kusini, Abdi Banda amesema mwaka huu ana
mpango wa kufungua kituo cha kukuza vipaji vya soka mkoani Tanga.
"Malengo
yangu ni kuwasaidia vijana wenzangu wa Kitanzania na mwaka huu
natarajia kufungua kituo cha kukuza vipaji jijini Tanga," amesema Banda.
Banda amesema atafanya hivyo kwasababu anatambua kuwa wapo vijana
wengi ambao wana ndoto za kufika mbali zaidi kisoka, hivyo wanahitaji
msaada kutoka kwa watu ambao wapo mbele katika soka.
''Unapocheza nje ya Tanzania ni vizuri kuonyesha mchango wako kwa
vijana walio chini yako, kwahiyo hilo ndio lengo langu na sitaishia tu
kujenga kituo nitaendelea kutoa vifaa vya michezo kwaajili ya vijana
wenye ndoto za kuwa wachezaji wakubwa'', ameongeza.
Banda alisajiliwa na Baroka FC kwenye usajili wa kiangazi Juni 2017,
baada ya kuonesha kiwango kizuri alipokuwa nchini Afrika Kusini na
kikosi cha Taifa Stars kwenye michuano ya COSAFA 2017. Baroka inashika
nafasi ya nne kwenye ligi kuu ya humo ikiwa na alama 22 baada ya
michezo15
Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania bara Yanga SC, imetangaza
fursa kwa vijana wenye vipaji vya soka kufanya usaili kwaajili ya
kusajiliwa na timu hiyo.
Bosi
wa benchi la ufundi la Azam FC, Aristica Cioaba, raia wa Romania na
wasaidizi wake, wanakoshwa na soka la mshambuliaji wao mpya, Bernard
Arthur raia wa Ghana ambaye amekuwa msaada mkubwa katika ushambuliaji.
Kapteni
wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, amewapoza mashabiki wa timu yake
kwa kuwaambia watulie kwani wao wachezaji wamejipanga kutwaa ubingwa wa
Kombe la Mapinduzi mwaka huu.
MSANII wa Bongo Fleva,
Pamela Daffa ‘Pam D’ amejikuta kwenye wakati mgumu wa kumfariji ndugu
yake ambaye pia ni msanii mwenzake, Mesen Selekta kutokana na kufiwa na
mama yake ambaye alimfia mikononi mwake.
Kaimu Kocha wa Simba, Masoud Djuma, akiamini Asante Kwasi
atawasaidia kutwaa mataji msimu huu, beki huyo amepania kufanya mambo
makubwa zaidi hasa kufunga mabao muhimu.