Saturday, November 18, 2017
WELBECK YUPO FITI KUIKABIRI SPURS LEO
Mshambuliaji Danny Welbeck akimruka kipa Petr Cech anayedaka mpira chini wakati wa mazoezi ya Arsenal jana viwanja vya Colney,
Singida United imepanda kwa nafasi moja
TIMU
ya Singida United imepanda kwa nafasi moja hadi ya tano baada ya
ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Lipuli ya Iringa kwenye mchezo wa Ligi Kuu
ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya Jana Uwanja wa Namfua, Singida.
MAHASIMU WA MADRID LEO
Mshambuliaji Cristiano Ronaldo akionekana mwenye kujiamini wakati wa mazoezi ya Real Madrid jana katika viwanja vyao vya mazoezi vya Valdebebas mjini Madrid, Hispania kujiandaa na mchezo wa leo wa La Liga dhidi ya Atletico Madrid Uwanja wa Wanda Metropolitano mjini Madrid
Dortmund yalala 2-1 dhidi ya Stuttgart.
Ikiwa inacheza mechi yake ya 12 ya Bundesliga, Borussia Dortmund imepoteza mchezo wake wa nne.
Dortmund ikicheza bila ya mshambulizi wake nyota, Pierre-Emerick Aubameyang imepigwa 2-1 dhidi ya Stuttgart.
Mechi
hiyo ilikuwa inarushwa moja kwa moja kupitia king'amuzi cha StarTimes
kinachoshika umaarufu mkubwa kwa sasa katika masuala ya michezo.
Haiwezekani hata kidogo Tambwe kuwa Mfungaji Bora....Kichuya
Kila mtu anakuwa na mawazo yake katika
jambo fulani, lakini kiungo nyota wa Simba, Shiza Kichuya anaweza
kutofautiana na wengi sana kuhusiana na Amissi Tambwe wa Yanga.
IRENE UWOYA KUHANI MSIBA WA NDIKUMANA KIGALI
rembo
wa zamani wa taji la Miss Chang’ombe na mwigizaji maarufu nchini, Irene
Uwoya amewasili jijini Kigali, Rwanda kuhani msiba wa aliyekuwa mumewe,
Ndikumana Hamad.
Sunday, November 12, 2017
Uwanja wa Taifa kukamilika November 21
Jana November 11, 2017 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akiambatana na kamati ya maandalizi ya fainali za Afrika (AFCON U17) amefanya ziara ya kutembelea uwanja wa taifa kukagua ukarabati unaoendelea katika eneo la kuchezea (pitch) na maeneo mengine.
Dkt. Mwakyembe ameishukuru kampuni ya SportPesa ambayo ndio imebeba jukumu la kukarabati uwanja huo.
“Nashukuru kuona nyasi za uwanjani zimeota vizuri na unapendeza, kikubwa nashukuru kwa vijana wetu sita ambao wamefundishwa namna ya kutunza viwanja”-Dkt. Mwakyembe.
Mkuu wa oparesheni SportPesa Luca Neghesti amethibitisha ukarabati wa uwanja utakamilika November 21 na utakabidhiwa November 24 mwaka huu ukiwa tayari kwa matumizi.
“Kazi ya kukarabati sehemu ya kuchezea imekamilika na nyasi zilizooteshwa zimeota vizuri na zimeshika hivyo upo tayari kutumika,” alisema Luca.
Vilabu vya Simba na Yanga ambavyo huutumia uwanja wa taifa kwa mechi zao za nyumbani huenda zikarejea kwenye uwanja huo kuanzia November 24 baada ya kukabidhiwa kwa serikali. Vilabu hivyo vililazimika kutumia uwanja wa Uhuru kwa mechi zao za nyumbani kupisha matengenezo yanayoendelea uwanja wa Taifa.
Neymar, aangua kilio mbele ya waandishi wa habari
Baada ya Brazil kuibuka kidedea kwa ushindi wa bao 3 dhidi ya Japan kulikuwa na mkutano baada ya mechi kati ya waandishi wa habari na nahodha wa Brazil Neymar pamoja na kocha mkuu wa timu hiyo Tite.
Katika mkutano huo jambo lililovuta hisia na kusikitisha mashabiki wa Brazil na PSG ni kitendo cha Mbrazil Neymar Dos Santos kuangua kilio na kisha kuamua kuondoka katika chumba cha mkutano.
Neymar aliangua kilio wakati kocha wake Tite akimzungumzia na akimtetea kuhusu habari zinazoandikwa siku za usoni kwamba hana furaha na maisha ya PSG na uhusiano wake na kocha wa klabu hiyo sio mzuri.
Tite amesema anakerwa sana na habari anazozishiwa Neymar ikiwemo kuwa na mahusiano mabaya na yeye kwani hajawahi kugombana na Neymar, wakati Tite akiendelea kumtetea Neymar ndipo alianza kulia.
Neymar mwenyewe kabla ya Tite kuongea alisisitiza kwamba ana furaha kuwa katika klabu ya PSG na kusema kwamba hana tatizo na mchezaji yoyote katika klabu hiyo, na yuko vizuri tu na Edison Cavani.
Alisisitiza kwamba kitu pekee kinamsumbua kwa sasa na kuambiwa hayuko vizuri na Edison Cavanni na amewataka waandishi wa habari kuacha kutunga story na kuandika vitu wasivyovijua.
Neymar alisajiliwa na PSG akitokea Barcelona kwa ada iliyovunja rekodi ya dunia ya £198m lakini tangu atue PSG amekuwa akitengeneza vichwa vingi vya habari na vingi vikiwa sio vizuri.
MBAO WANAAMINI WATAZINDUKA NA KUDHIHIRISHA UBORA WAO VPL
MWENYEKITI
wa Mbao FC, Solly Zephania Njashi amesema kwamba anaamini timu yake
itazinduka na kufanya vizuri katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
MOROCCO WAFUZU KOMBE LA DUNIA
TIMU
ya taifa ya Morocco imekata tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia
mwakani nchini Urusi baada ya kuwapiga wenyeji, Ivory Coast mabao 2-0
mjini Abidjan.
MO KUTOFURAHIA MAISHA YA TIMU YAKE
Kiungo Mohamed Ibrahim wa Simba, ameichezea timu yake mechi ya kirafiki iliposhinda kwa mabao 3-1 dhidi ya Rukwa FC.
BALE AMEKOSA MECHI 79 TOKA ATUE MADRID
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiVf3ANYbu1C2gk5RPLgOs1qRcdnBK4gns7kc14td61Ilb8V8tmRoONSgkG26OAMLPDGjZb-a-LypMvwzYBpV2ua8XvEecVG_CiEdIZ5Bv24kS1d125IRPXxodZTn64RuM6ZBPljJ66UVpD/s400/bale+madirid.jpg)
Tokea amejiunga na Real Madrid Juni, 2013 kiungo Gareth Bale, ameumia na kulazimika kukaa nje ya uwanja mara 24.
Alianza kwa kuumia nyama, baadaye ikafuatia enka na akalazimika kufanyiwa upasuaji.
Kutokana na kuandamwa na majeraha mara kwa mara alishindwa kucheza mechi 17 mfululizo katika msimu wa 2016/17.
Kabla ya hapo katika msimu wa In 2015/16, Bale alikosa mechi 19 katakana na tatizo la nyama au misuli.
Msimu wa 2013/14, akiwa mbichi kabisa alikosa mechi 15 kutokana na tatizo hilo la misuli.
Kama utazungumzia mechi za mashindano ambazo amekosa tokea amejiunga na Real Madrid akitokea Tottenham ya England, ni 79.
Saturday, November 11, 2017
URENO YAWAPIGA 3-0 SAUDI ARABIA,
Beki wa kati, Pepe akimpongeza Manuel Fernandes baada ya kuifungia Ureno dakika ya 32 katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Saudi Arabia usiku wa jana Uwanja wa Manispaa
ya Fontelo mjini Viseu. Mabao mengine ya Ureno iliyomkosa nyota wake,
Mwanasoka Bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo yalifungwa na Goncalo Guedes
dakika ya 52 na Joao Mario dakika ya 90
SENEGAL WAFUZU KOMBE LA DUNIA
TIMU
ya soka ya taifa ya Senegal imekata tiketi ya fainali za kombe la Dunia
mwakani nchini Urusi baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji,
Afrika Kusini Uwanja wa Peter Mokaba mjini Polokwane jana.
WACHEZAJI VPL HATARINI KUTEMWA HEROES
Wachezaji wa timu ya Taifa ya Soka ya Zanzibar (Zanzibar Heroes), ambao wanacheza ligi kuu Tanzania bara huenda waachwa katika kikosi hicho kutokana na kutopewa ruhusa na vilabu vyao kujiunga na timu hiyo ya Taifa mpaka ligi kuu bara itakapokwenda mapumziko.
ITALY WAKALIA KUTI KAVU KUELEKEA URUSI 2018
Timu ya taifa ya Ubelgiji ilikuwa uwanjani usiku wa jana kukabiliana na
timu ya taifa ya Mexico ambapo katika mchezo huo Romelu Lukaku alifunga
mabao mawili kati ya matatu katika suluhu ya tatu tatu.
MSULULU WA MAJERUHI KUONGEZEKA MANCHESTER UNITED
Taarifa zinasema Paul Pogba na Marcos Rojo wako mbioni kurejea uwanjani na mwisho wa wiki hii wanaweza kuwepo uwanjani katika kikosi cha Manchester United.
Jamhuri Kihwelo lazima nisajili
Itakapofika Novemba 15, mwaka huu ndipo dirisha dogo la usajili ndipo litakapofunguliwa, sasa Kocha wa Dodoma FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’
YANGA YASISITIZA WASIO FITI HAWATAKUWA NA NAFASI
Uongozi wa Yanga umesema unataka wachezaji wanaojituma na wenye nia ya kuisaidia klabu.
NDEMLA KUANZA MAJARIBIO JUMATATU AFC
Kiungo Said Hamis Ndemla anatarajia kuanza majaribio katika klabu ya AFC, keshokutwa Jumatatu.
Sunday, November 5, 2017
Deontay Wilder anamtaka Anthony Joshua.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgVbWmaqF-lKSAVtzbD9GuVVBkMBSEv9e_m9lEdK580OWL5k4sqT0ldLW_FBj731EfNQppF4GO8_giLvHHkZyENgT6H_QKdKm9BEkOzFW7aVY4R7-ae77JcKZ32A7rEFgE8jMk9JWQGEony/s400/4606A2D600000578-5051081-image-m-8_1509860732953.jpg)
Deontay Wilder amemtwanga Bermane
Stiverne katika pambano lao la uzito wa juu na baada ya kutangazwa
mshindi, akasema waziwazi kwamba sasa anamtaka Anthony Joshua.
Wilder ameshinda katika raundi ya kwanza tu baada ya kumvurumishia mpinzani wake makonde utadhani mvua za masika.
Sasa anachotaka ni kumvaa Joshua raia wa Uingereza ili kumaliza ubishi.
Ubishi mkubwa upo kati ya Mmarekani huyo na Muingereza huyo nani ni mkali zaidi.
Lakini kipigo kikali alichotoa Wilder
kwa Stiverne kinafanya wengi waaamini atakuwa maji marefu kwa Joshua
lakini wako wanaosisitiza Joshua ni Joshua lakini lazima aimarishe
kiwango chake kwanza.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjgtDfLF8CJro-vzRwqWaaLYeQqS1T4cjl9diU6gWgiOqDZIXcx1LP_2pc3H3B3reyO2XkahEpWinIW-VSqb3m7ZII4iEvKuMlKcaDGvKJYCOimYtsa5856acj30TsiOWP56DlCzyYRw5AR/s400/4606B19600000578-5051081-image-m-18_1509861004833-1.jpg)
MATOKEO YA MECHI ZA EPL
Saturday 04 November | ||||||
FT | Stoke | 2 - 2 | Leicester | |||
FT | Huddersfield | 1 - 0 | West Bromwich | |||
FT | Newcastle | 0 - 1 | Bournemouth | |||
FT | Southampton | 0 - 1 | Burnley | |||
FT | Swansea | 0 - 1 | Brighton | |||
FT | West Ham | 1 - 4 | Liverpool | |||
Sunday 05 November | ||||||
FT | Tottenham | 1 - 0 | Crystal Palace | |||
FT | Manchester City | 3 - 1 | Arsenal | |||
FT | Chelsea | 1 - 0 | Manchester United | |||
FT | Everton | 3 - 2 | Watford |
SIMBA YARUDI KILELENI LIGI KUU
Kabla ya mchezo huo, Simba ilikuwa nafasi ya nne nyuma kwa pointi moja kwa Yanga na Mtibwa zilizotoka suluhu kwenye mechi zao za jana lakini ilikuwa imezidiwa pointi tatu na Azam ambayo ilishinda dhidi ya Ruvu Shooting.
Uhindi wa Simba dhidi ya Mbeya City umeipa Simba pointi tatu na sasa imefikisha pointi 19 sawa na Azam lakini Simba inaonoza ligi wastani wa magoli dhidi ya Azam.
- Kichuya amefikisha magoli matano (5) kwenye ligi sawa na Ibrahim Ajib wa Yanga huku akiwa anaziwa na Mohamed Rashid wa Tanzania Prisons mwenye magoli sita na Emanuel Okwi wa Simba anaeongoza akiwa na magoli nane.
- Simba imeshinda mechi ya tatu kati ya tano ilizokutana na Mbeya City kwenye uwanja wa Sokoine, Mbeya. Kabla ya mchezo wa leo, Simba ilikuwa imeshinda mechi mbili kati nne, mchezo mmoja walitoka sare na mwingine walipoteza.
- Mbeya City imepoteza mchezo wa pili kati ya mechi tano walizocheza kwenye uwanja wa Sokoine. Mchezo mwingine waliopoteza kwenye uwanja wa Sokoine ilikuwa dhidi ya Ndanda.
- Simba imeshinda mechi yake ya pili nje ya uwanja wa Uhuru ambao ndio uwanja wao wa nyumbani.
Brenden Rodgers aweka rekodi kubwa na Celtic,
Kocha wa zamani wa Liverpool Brenden Rodgers ameweka rekodi ya kuwa kocha wa kwanza kuifanya timu kutoka Uingereza kucheza michezo 63 ya ligi ya ndani bila kupoteza.
Kikosi cha Celtic kimeshinda michezo 56 na kusuluhu 7 wakiwa wamefunga mabao 183, wakifungwa 35 na kucheza michezo 36 bila nyavu zao kuguswa.
Lakini pamoja na Rodgers kuwapa Celtic rekodi hiyo tayari kuna vilabu ambavyo vimecheza mechi nyingi zaidi katika ligi zao bila kupoteza mchezo hata mmoja.
1.Steaua Bucharest. Hakuna klabu dunianj inayofikia rekodi ya timu hii kutoka Romania,mwaka 1986 wakati wakibeba kikombe cha European Cup walicheza michezo 119 ya ndani hadi mwaka 1989 ndipo wakapoteza mchezo.
2.Lincolin Red Imps. Mwaka 2009 mwezi May hadi September mwaka 2014 walicheza michezo 88 ya ligi ya kwao bila kupoteza mechi na pia wamewahi kuchukua makombe 14 mfululizo ya ligi nchini kwao Gibraltar.
3.Ac Millan. Kati ya mwaka 1991 na 1993 klabu soka ya Ac Millan ilichukua makombe matatu mfululizo, lakini si hivyo tu bali pia Millan walicheza michezo 58 ya ligi ya kwao bila kupoteza hata mmoja.
4.Ajax. Ajax iliyochukua ubingwa wa Champions League mwaka 1995 ilikuwa kati ya Ajax bora kuwahi kutokea,mwaka ambao wanachukua kombe hilo walicheza michezo 52 bila kupoteza mchezo hata mmoja.
5.Arsenal. Wengi wanaikumbuka Arsenal hii ya nwaka 2003 ambapo hadi inafima 2004 mwezi October walikuwa hawajapoteza mchezo na Manchester United ndio walikatisha safari yao ya michezo 49 bila ushindi
City waendelea kuweka rekodi mpya
Mchezo wa pili kati ya michezo kumi iliyopita Pep Gurdiola anapata
ushindi zidi ya Arsenal ushindi ambao unawafanya Manchester City
kuendelea kutawala katika ligi ya Epl.
Manchester United yalala mbele ya Chelsea 1-0
Manchester United wameendeleza rekodi mbovu dhidi ya timu kubwa baada ya hii leo Jose Mourinho kupoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya mabingwa watetezi.
Manchester United kuwafuata chelsea darajani
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgAkn9eUYcZq6OV4mjFyc9uuijzrY7doFsbv4uUvaM7pkKDPyTAtz24y8nhd22Xa837PezQsi3QK3dAUXXxgFt9-nzpqGjRbh0uUh47EGz7hClwM04rM9APXo9eXCj-PUAMFBTq3gpJ-FM-/s400/46016A6600000578-0-image-a-61_1509809081419.jpg)
Manchester United wamekwea treni hadi jijini London na tayari wamewasili.
Kutoka Manchester hadi London ni mwendo wa saa mbili na dakika 5 hadi 15 na kilichowaplekeka ni shughuli ya leo.
Man United wan a kazi darajani, yaani Stamford Bridge watakapowavaa wakali Chelsea.
Kazi
haitakuwa rahisi na Manchester lazima washinde kuhakikisha hakuna pengo
kubwa kati yao na Manchester City ambao wameisshaanza kuwaacha.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgnjrdnXBIysjEfUbb1QNPTnk_y9py-noGAyBbA0OH1U77_gijwYKp3i9243GHXHoclQ95pMv7Z7ZwI32CdRk0MDw92gPKoD3XouugwFfjsEYmZafjDYHahKEvcdLIJ3gHovTO1z-tC8G21/s1600/46014CB600000578-0-image-m-52_1509808518748.jpg)
ARSENAL WAKO TAYARI KWA KIBARUA CHA LEO
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhP7YvQFhEhhU4r7u6u2mCF1Wyv0Wbcit6aen3Sawx2cqq8XWL9wQlI_-hCuRu3ngp6g5jpSSeXyVK8PILTw7KkHGdiZXoHYmCFW3HuD52JBgGs4V_xmiDb6Qap1uLxWesBatd8W9dZhc6J/s400/46022D4C00000578-0-image-a-2_1509813274533.jpg)
Arsenal wamesafiri hadi jijini Manchester kwa mechi yao ya leo dhidi ya Manchester City.
Katika mazoezi yao, wameonekana ni wenye furaha na wako tayari kwa ajili ya mchezo huo.
Mechi
tatu zilizopita zinaonyesha sare mbili na moja Arsenal walipoteza.
Inawezekana ikawa nafasi yao nzuri kujisogeza katika nafasi nzuri katika
msimamo wa Ligi Kuu England.
Lakini haitakuwa mechi rahisi na lazima vijana wa Arsene Wenger wafanye kazi ya ziada.
Subscribe to:
Posts (Atom)