Sunday, October 22, 2017

AGUERO AMEIFIKIA REKODI YA ERIC BROOK BAADA YA KUIBAMIZA 3-0 BURNLEY


Sergio Aguero akishangilia baada ya kuifungia bao la kwanza Manchester City kwa penalti dakika ya 30 baada ya Nick Pope kumchezea rafu Bernardo Silva wakiichapa 3-0 Burnley kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Etihad. Hilo ni bao la 177 kwa Aguero Man City, maana yake ameifikia rekodi ya Eric Brook aliyoweka miaka ya 1930. Mabao mengine ya City yamefungwa na Nicolas Otamendi dakika ya 73 na Leroy Sane dakika ya 75

No comments:

Post a Comment