Saturday, October 14, 2017

Getafe kumpa Zinedine Zidane rekodi mpya Real Madrid


Hakuna aliyedhani kwamba Zinedine Zidane anaweza kuwa kati ya makocha wakubwa duniani, wengi waliamini Zidane asingeiweza Real Madrid na wakiamini baada ya muda anaweza kutimuliwa.

Lakini tangu January 4 2016 wakati Perez akimkabidhi timu Zidane amekuwa akiwaonesha watu kwamba haikuwa bahati mbaya kupewa Real Madrid na ilikuwa sahihi kwake kupewa timu.
Kwa sasa Zinedine Zidane siyo yule ambaye siku 600 zilizopita wachambuzi wengi duniani walikuwa hawaamini kwamba atafanya vizuri kwani sasa anatajwa kama mmoja wa makocha bora duniani.
Wikiendi hii Zinedine Zidane anaweka rekodi katika klabu ya Real Madrid ambapo mchezo wake wa leo dhidi ya Getafe utamfanya Mfaransa huyo kufikisha idadi ya mechi 100 tangu apewe ukocha mkuu.
Takwimu zinaonesha Zinedine Zidane ni kocha aiyefanya makubwa zaidi Real Madrid akiweka rekodi kuwa kocha wa kwanza kutetea Champions League na katika michezo yake 100 ameipa Madrid makombe 7.
Zinedine Zidane ndiye kocha aliyekata kiu ya miaka mitano ya Real Madrid kuchukua ubingwa wa La Liga huku akiwapa pia Europeans Cup mara mbili, klabu bingwa dunia na Spanish Super Cup.

No comments:

Post a Comment