Sunday, October 22, 2017

NANI KAPELEKA UCHAWI UKEREWE ?



   NINI CHANZO NA ASILI YA UCHAWI KATIKA KISIWA CHA UKEREWE ?...
Kwa mujibu wa utafiti, mpaka mwaka 1500, kisiwa cha Ukerewe hakikuwa kinakaliwa na watu.
Yaani kwa lugha ya kitaalamu zaidi , tunaweza kusema, kisiwa cha Ukerewe kilikuwa TERRA NULIUS. Hakukuwa na mtu yoyote aliyekuwa anaishi kwenye kisiwa cha Ukerewe zaidi ya kuwa pori kubwa linalo kaliwa na wanyama wa mwituni. Wavuvi wachache kutoka katika maeneo ya Mwanza, Sengerema( Uvinza), Kagera na Mara walikuwa wanapita katika kisiwa hicho katika shughuli zao za uvuvi
WATU WALIANZA VIPI KUISHI UKEREWE
Rekodi zinaonyesha kuwa, kisiwa cha Ukerewe kimeanza kukaliwa na watu mwishoni mwa miaka ya 1700 au mwanzoni mwa miaka ya 1800. katika kipindi chote ambacho kisiwa cha Ukerewe hakikuwa kinakaliwa na watu, wachawi kutoka Gamboshi na maeneo mbalimbali ya kanda ya ziwa kama vile Mwanza, Shinyanga, na mikoa ya Tabora, Singida na Kigoma, walikuwa wanakitumia kisiwa cha ukerewe kama himaya ya kufanya shughuli zao za kichawi.
Wachawi hawa hawakuwa wakiishi katika kisiwa hicho, bali waliishi katika maeneo mbalimbali ya kanda ya ziwa, ila kisiwa cha ukerewe walikitumia kwa ajili ya kufanya shughuli zao mbalimbali za kichawi kama vile kufuga misukule. Kufanya ibada za kichawi, kuwalimisha watu kichawi, kufanya kafara za kichawi nakadhalika.
Watu wa kwanza kwenda kuishi katika kisiwa cha ukerewe walikuwa ni wavuvi wakifuatiwa na wakulima kisha wafanyabiashara kutoka katika maeneo ya Mwanza, Sengerema, Majita na Bukoba. Hii kwa lugha nyingine ni sawa na kusema kuwa kisiwa cha ukerewe kilianzishwa na wavuvi na wakulima kutoka katika mikoa ya Mwanza, Kagera & Mara.
Nadharia hii inasema kuwa watu wa kwanza kufika katika kisiwa cha Ukerewe walikuwa ni wavuvi kutoka katika mkoa wa Mwanza. Wavuvi hawa walifika katika kisiwa cha Ukerewe wakiwa katika harakati zao za kutafuta eneo lenye samaki wengi.
Inasemekana kuwa , wavuvi hawa walifurahishwa sana na uwingi wa samaki waliokuwa wanapatikana katika kisiwa cha Ukerewe, ambapo waliamu kupiga kambi yao kabisa katika kisiwa hicho na biashara yao ikawa ni kuwatoa samaki Ukerewe na kuwapeleka Mwanza, Mara na Bukoba.
Baadaye wavuvi wengine pamoja na wafanyabiashara wa samaki kutoka Mwanza , Mara na Kagera nao waliamua kwenda kuweka makazi yao katika kisiwa hicho baada ya kupata sifa zake nzuri.. Kutokana na ardhi yake kuwa nzuri na yenye rutuba, wakulima kutoka katika mkoa wa Mwanza walianza kufanya shughuli za kilimo katika kisiwa hicho, wakijikita zaidi katika mazao ya nyanya, mbogamboga kama vile mchicha, pamoja na machungwa kwa kutaja vichache.
Sifa nzuri za kisiwa cha ukerewe ziliendelea kusambaa na kuzidi kuwavutia wana kanda ya ziwa ambapo sasa wakaanza kumiminika kwa wingi wao katika kisiwa hicho kwa ajili ya kuweka makazi yao na kufanya biashara zao.
 Watu hawa ndio walio peleka uchawi katika kisiwa cha Ukerewe walio toka nao katika jamii zao. Inafahamika kuwa wavuvi ni watu wanao jihusisha sana na masuala ya ushirikina ili waweze kuendelea kufanya shughuli zao za uvuvi bila maruweruwe, hivyo basi tunapo zungumzia aina ya uchawi hapa, tunazungumzia uchawi mkubwa kutoka kwenye madhabahu kubwa ya kichawi

No comments:

Post a Comment