KOCHA
wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Salum Mayanga amewarejesha
kikosini kiungo Farid Mussa na mshambuliaji, Elias Maguri kwa ajili ya
mchezo wa kirafiki wa kimataifa mapema mwezi ujao.
Baada
ya kucheza nyumbani mfululizo mechi za kirafiki za kimataifa, Taifa
Stars sasa itatoka mwezi ujao kwenda Benin kucheza na wenyeji Novemba
11, mwaka huu.
Na
Mayanga leo ameita kikosi cha wachezaji 24 ambacho kitaingia kambini
Novemba 5 mjini Dar es Salaam kabla ya kusafiri Novemba 9 kwenda Benin
tayari kwa mchezo huo.
Na
ndani yake amewaorodhesha Maguri aliyekuwa anacheza Oman na Farid Mussa
anayecheza Tenerife B ya Hispania, ambao wote hakuwaita kwenye mchezo
uliopita dhidi ya Malawi, uliomalizika kwa sare ya 1-1 Oktoba 7, Uwanja
wa Uhuru, Dar es Salaam.
Kikosi
kamili cha Taifa Stars kilichotajwa leo kinaundwa na makipa; Aishi
Manula (Simba SC), Peter Manyika (Singida United) na Ramadhani Kabwili,
mabeki Boniphace Maganga (Mbao FC), Abdi Banda (Baroka FC/Afruka
Kusini), Gardiel Michael (Yanga), Kevin Yondan (Yanga), Nurdin Chona
(Prisons), Erasto Nyoni (Simba) na Dickson Job (Mtibwa Sugar).
Viungo
ni Himid Mao (Azam FC), Hamisi Abdallah (Sony Sugar/Kenya), Muzamil
Yassin (Simba), Raphael Daudi (Yanga), Simon Msuva (Yanga), Shiza
Kichuya (Simba), Ibrahim Hajib (Yanga), Mohammed Issa (Mtibwa), Farid
Mussa (Tenerife/Hispania) na Abdul Mohammed (Tusker/Kenya) na
washambuliaji Mbwana Samatta (KRC Genk/Ubelgiji), Mbaraka Yussuf (Azam
FC), Elias Maguri (Huru) na Yohanna Nkomola (Huru).
No comments:
Post a Comment