AZAM
FC imepanda kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya
ushindi wa 1-0 dhidi ya Mbeya City usiku huu Uwanja wa Azam Complex,
Chamazi, Dar es Salaam.
Bao
hilo lilitokana na makosa ya kipa Mmalawi wa Mbeya City, Owen Chaima
aliyetema mpira wa kona ya Enock Atta Agyei dakika ya 59 ukamgonga
mshambuliaji wa Azam FC, Mbaraka Yusuph na kuingia ndani.
Beki
Hassan Mwasapili akajaribu kuokolea ndani mpira huo kwa kuupiga
kuurudisha mchezoni, lakini refa Ole Yangalai Shakalai hakudanganyika na
akawapa haki yao Azam FC.
Kwa
ushindi huo, Azam FC inapanda kileleni mwa Ligi Kuu japo kwa muda tu
ikifikisha pointi 16, baada ya kucheza mechi nane – ikizizidi kwa pointi
moja moja, Simba, Yanga na Mtibwa Sugar zinazofungana katika nafasi ya
pili sasa, ingawa zote zina mchezo mmoja mkononi.
Simba
na Yanga zitamenyana zenyewe kwa zenyewe Leo Uwanja wa Uhuru, Dar es
Salaam wakati, Mtibwa Sugar watakuwa wenyeji wa Singida United
inayoshika nafasi ya tano kwa pointi zake 12.
Kikosi
cha Azam FC kilikuwa: Razak Abalora, Daniel Amoah, Bruce Kangwa, Aggrey
Morris, Yakubu Mohammed, Bryson Raphael, Himid Mao, Salum Abubakar
‘Sure Boy’/Iddi Kipagwile dk68, Mbaraka Yusuph/Frank Domayo dk83, Enock
Atta Agyei na Yahya Zayed/Yahya Mohammed dk73.
Mbeya
City: Owen Chaima, Erick Kyaruzi, Hassan Mwasapili, Ally Lundega,
Sankan Mkandawile, Babu Ally, Mrisho Ngassa/Iddi Suleiman dk70, Mohammed
Samatta, Frenk Ikobelo/Omary Ramadhani dk70, Mohammed Mkopi/Anthony
Mwingira dk86 na Eliudi Ambokile.
No comments:
Post a Comment