Niyonzima amezungumza na Dossantostz na kusema kiwango chake hakijawa kama anavyotaka.
"Kweli sijafikia kama ninavyotaka, ndiyo maana nimeamua kufanya mazoezi ya ziada.
"Nafanya hivyo ili kuwa katika kiwango
ninachotaka. Hii inatokana na kwamba sikupata muda mzuri wa mazoezi
mwanzoni mwa msimu," alisema.
Niyonzima alichelewa kujiunga na kikosi
cha Simba na alishindwa kujiunga nacho wakati kikiwa kambini nchini
Afrika Kusini kujiandaa na msimu mpya.
Wakati huo ndiyo alikuwa amejiunga na
Simba akitokea Yanga lakini alibaki nchini kwao Rwanda kwa ruhusa ya
uongozi wa Simba kwa kuwa alikuwa akisomea ukocha.
No comments:
Post a Comment