Sunday, October 8, 2017

Mkongwe wa Afrika akaribia kuweka rekodi kombe la dunia 2018



Essam El Hadary ni miongoni mwa magolikipa bora wa Afrika. Anatarajia kushiriki michuano ya kombe la dunia 2018 baada ya kuiongoza
Misri kufuzu kufuatia ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Essam anatarajiwa kuwa mchezaji mwenye umri kubwa zaidi katika fainali za kombe la dunia zitakazofanyika Russia.
Kwa sasa mchezaji anaeshikilia rekodi ya kuwa mchezaji mwenye umri mkubwa aliyewahi kushiriki fainali za kombe la dunia ni raia wa Columbia Faryd Mondragon ambaye alikuwa na miaka 43 alipocheza fainali za kombe la dunia za mwaka 2014 nchini Brazil.
Hivi karibuni, Essam El Hadary ataivunja rekodi hiyo na kuweka rekodi yake ambapo atakuwa na miaka 45 wakati wa fainali zijazo za kombe la dunia 2018 lakini hiyo itakuwa endapo atafanikiwa kucheza katika fainali zijazo za kombe la dunia.
Mshindi huyo wa mataji manne ya Afrika (1998, 2006, 2007 na 2010) amesema atapambana kuhakikisha anacheza fainali za kombe la dunia, Essam alikuwepo kwenye kikosi kilichoshiriki fainali za kombe la mataifa ya Afrika mwaka huu akiwa ni mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi.

No comments:

Post a Comment