Uongozi wa Klabu ya Simba umemuweka sokoni kiungo mshambuliaji wake, Shiza Kichuya kwa kukaribisha ofa kutoka klabu yoyote.
Hivi
karibuni Klabu ya Ismailia ya Misri ilishindwana na Simba juu ya dau la
kumuuza kiungo huyo ambalo lilikuwa dogo, hivyo kusababisha uongozi wa
klabu hiyo kukataa.
Kichuya
ni miongoni mwa wachezaji wa Simba ambao wanacheza kwa kiwango kizuri
na kuisaidia timu yake hiyo, jambo ambalo timu nyingi zimekuwa
zikimnyemelea.
Ofisa
Habari wa Simba, Haji Manara, amefunguka kuwa, dili lao na Ismailia juu
ya kumchukua Kichuya limekufa rasmi, lakini wamemuweka sokoni mchezaji
huyo kwa timu yoyote itakayomhitaji.
“Ile
dili kati yetu na Ismailia ilishakufa rasmi kwa sasa hakuna ishu ya
Kichuya kwenda huko, lakini tupo tayari kupokea ofa yoyote ile, iwapo
kuna timu itamhitaji tutakuwa tayari kumuuza mchezaji huyo.
“Simba
tumekuwa na desturi ya kuwaachia wachezaji wetu kuwauza pale
tunapofanikiwa kupata timu ya kucheza, hivyo mchezaji yeyote yule
atakayetakiwa tutakuwa tayari kumuachia,” alisema Manara.
No comments:
Post a Comment