Kamati mpya ya Uongozi ya Bodi ya Ligi
Kuu (TPLB) inafanya kikao chake cha kwanza Alhamisi, Oktoba 26 mwaka huu
jijini Dar es Salaam.
Moja ya ajenda katika kikao hicho ni kuteua Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi, na kamati nyingine mbalimbali.
TPLB ilifanya uchaguzi Jumapili, Oktoba 15 mwaka huu na kupata uongozi mpya chini ya Mwenyekiti wake Clement Sanga.
Viongozi wengine waliochanguliwa ni
Shani Mlingo (Makamu Mwenyekiti) na wajumbe Hamisi Madaki, Ramadhani
Mahano, Almasi Kasongo na Egdar Chibura.
Boniface Wambura
Ofisa Mtendaji Mkuu
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB)
No comments:
Post a Comment