WINGA
wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva usiku huu ameisaidia
timu yake, Difaa Hassan El-Jadida kupata ushindi wa mabao 2-1 ugenini
kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Morocco, maarufu kama Botola dhidi ya
wenyeji FAR Rabat Uwanja wa Prince Moulay Abdallah mjini Rabat.
Katika
mchezo wa leo, Msuva alianzia benchi na baada ya dakika 45 za kipindi
cha kwanza kumalizika timu hizo zikiwa hazijafungana, Difaa wakafanya
mabadiliko.
Na
miongoni mwa wachezaji walioingia ni winga wa zamani wa Yanga, Simon
Happygod Msuva, mfungaji bora mara mbili na mchezaji bora mara moja wa
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Hata
hivyo, ni wenyeji FAR Rabat waliotangulia kupata bao kupitia kwa kiungo
Mohamed El Fakih dakika ya 52, kabla ya Bilal Al-Makri kuisawazishia
DHJ dakika ya 55.
Shujaa
wa Difaa Hassan El- Jadida leo ni Hamid El Ahadad aliyefunga bao la
ushindi dakika ya 90 na ushei na kuwanyamazisha mashabiki wa timu
wenyeji.
Ilikuwa
ni furaha kubwa kwa Msuva na wachezaji wenzake baada ya mechi hiyo
kutokana na ushindi huo wa ugenini dhidi ya moja ya timu tishio Morocco
na Kaskazini mwa Afrika kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment