Mshambuliaji
Walid Azarou alifunga mabao matatu (hat-trick) kwenye ushindi wa mabao
6-2 ilioupata Al Ahly. Mabao mengine ya Al Ahly yalifungwa na Ali
Maaloul pamoja na Rami Rabiaa huku Hamdi Naguez wa Etoile du Sahel
akifunga na kukamilisha mabao 6 ya Ahly.
Al Ahly imeshinda kwa jumla ya mabao 7-4 na kutinga fainali ambapo sasa itacheza na Wydad Casablanca ya Morocco.
Al Ahly ni mabingwa wa Kihistoria wa
ligi ya mabingwa Afrika wakiwa wametwaa kombe hilo mara 8 na endapo
wataifunga Wydad Casablanca wataongeza rekodi yao.
Wydad Casablanca watakuwa wanatafuta
taji la pili la ubingwa wa Afrika ambapo mara ya mwisho walitwaa mwaka
1992 kabla ya kupoteza fainali mwaka 2011 dhidi ya Esperance.
No comments:
Post a Comment