Matokeo rasmi ya uchaguzi nchini Liberia hayajatangazwa, lakini taarifa za awali zinadai kwamba George Weah yupo katika nafasi nzuri ya kushinda uraisi huku kura zake zikikaribiana na mpinzani wake Joseph Boakai.
Weah ambaye alizaliwa katika mji wa Monrovia nchini Liberia miaka 51 iliyopita mjini Monrovia katika jimbo la Grand Kru lililopo kusini mwa Monrovia mahali ambapo kunatokea watu wa hali ya chini sana nchini Liberia.
Pamoja na umaskini lakini haikumzuia Weah kupiga soka na rasmi alianza mwaka 1984 ambapo alikuwa akicheza moja katika timu ya mtaani kwao iitwayo Mighty Ballore na kutwaa kombe la Liberia 1985.
Baadaye akakipiga Invincible Eleven ya nchini humo na akabeba tena kombe la Liberia kisha akaenda Tounare Younde ambapo hapo ndipo safari ya Ulaya ilianza alipouzwa kwenda Monaco mwaka 1992.
Weah ambaye aliwahi kuwa mkristo akaenda uislam kisha kurudi tena ukristo maisha yake ya Monaco alicheka na nyavu mno kwani katika misimu minne aliyokuwa hapo alipasia kamba mara 47 na hapo ndipo vilabu vikaanza kupigana vikumbo kutaka kumnunua.
Msimu wa mwaka 1992/1993Weah alivaa jezi ya PSG ambapo alikipiga hadi msimu wa 1997/1998 na katika misimu aliyokuwa hapo alifunga jumla ya mabao 56 na kubeba makombe manne na mwaka 1995 akawa mchezaji wa kwanza na wa mwisho kubeba tuzo ya Ballon D’Or toka Afrika.
Weah alienda Ac Millan na kujaribu maisha katika Serie A nako akafunga mabao 46 na kubeba Serie A mara mbili kabla ya kutimkia Chelsea alikobeba kombe la FA mwaka 2000 na kisha Manchester City.
Kiujumla Weah aliweka kambani jumla ya mabao 134 tangu ameanza kucheza soka la barani Ulaya huku akibeba tuzo ya mchezaji bora wa Afrika mara 3 na kutokea katika kikosi bora cha FIFA mara 4, 1194/1995 aliibuka kidedea katika Champions League kama mfungaji bora.
Safari yake ya siasa ilianza mwaka 2005 ambapo Weah ndipo alipotangaza kuingia kwenye mbio za uraisi kupitia chama cha Congress For Democratic Change huku wananchi wengi wakionekana kumkubali.
Pamoja na Weah kupambana sana hadi kufika hapa alipo lakini nchini kwao wapinzani wamekuwa wakitumia kigezo cha kutokuwa na elimu kama kampeni ya kumpinga, matokeo rasmi ya uchaguzi Liberia yanatarajiwa kutoka baadae hii leo.
No comments:
Post a Comment