Kupitia
ukurasa wake wa mtandao wa picha (Instagram) Manara ameandika ujumbe wa
kumsifia mshambuliaji wa timu hiyo Emmanuel Okwi akimfananisha na
Cristiano Ronaldo.
Aidha Haji Manara ameenda mbali zaidi na
kuhusisha namba ya jezi ya Okwi na idadi ya mabao ambayo Simba
itaifunga Yanga kwenye mchezo huo.
“Aliyeshinda tuzo ya FIFA anavaa namba
saba, anaeongoza kwa kufunga nchini anavaa namba saba, Emanuel na
Ronaldo zina herufi saba, Jumamosi ni siku ya saba ya wiki, tarehe 28
ukiigawa kwa kwa nne (idadi ya herufi za jina la Okwi) unapata saba,
nimejipigia hesabu tu, ukibisha kasomee upishi”.
Yanga na Simba zinakutana kwenye raundi
ya nane ya Ligi kuu soka Tanzania bara siku ya Jumamosi Oktoba 28 kwenye
uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam ambapo Yanga itakuwa mwenyeji wa
mchezo huo.
No comments:
Post a Comment