![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjpAX13X6qqtJoKoVv9I2zuOcyFERQKvpCkxNJeRlbQUi-x4Wer2sooDJCz89D6oSqQueeyDcyDXOBV5a42nMD3yw3XdlvP7jvnTLUs1cQNX1SMkH_eQ9FCrdDxrTVCM19sA4iCvOrrXT5z/s400/1.jpg)
Mahakama
nchini Afrika Kusini imetupilia mbali rufaa iliyokuwa imewasilishwa na
Rais Jacob Zuma kupinga kufufuliwa kwa mashtaka ya ulaji rushwa dhidi
yake.
Zuma
pamoja na maafisa wengine wakuu wa serikali walituhumiwa kupokea rushwa
wakati wa ununuzi wa ndege za kivita, maboti na silaha nyingine.
Mwaka
2005 mfanyabiashara Shabir Shaik alituhumiwa kupokea rushwa kutoka
katika kampuni inayouza silaha ya Ufaransa kwa niaba ya Zuma lakini rais
Zuma amekuwa akisisitiza kwamba hana hatia.
Mashtaka
hayo yaliwasilishwa mara ya kwanza dhidi ya Jacob Zuma mwaka 2005
lakini yakaondolewa na waendesha mashtaka mwaka 2009 na kumuwezesha Zuma
kuwania urais.
Mwaka
jana Mahakama Kuu mjini Pretoria iliamua kwamba kiongozi huyo anafaa
kujibu mashtaka hayo dhidi ya rais Zuma ambaye anamaliza muda wake wa
uongozi mwaka 2019.
Katika kipindi ambacho amekuwa madarakani, amekabiliwa na kura ya kutokuwa na imani naye mara nane, na kunusurika.
Ndiye
rais aliyenusurika majaribio mengi zaidi ya kutaka kumuondoa madarakani
Afrika Kusini tangu kumalizika kwa utawala wa ubaguzi wa rangi mwaka
1994.
No comments:
Post a Comment