Saturday, October 28, 2017

KANE NJE MECHI NA MAN UNITED KESHO

 












MATOKEO YA MECHI ZA SPURS BILA KANE MSIMU ULIOPITA

Middlesbrough 1-2 Tottenham
Tottenham 2-0 Manchester City
West Brom 1-1 Tottenham
Bournemouth 0-0 Tottenham 
Tottenham 1-1 Leicester
Tottenham 2-1 Southampton
Burnley 0-2 Tottenham
Swansea 1-3 Tottenham
TIMU ya Tottenham imepata pigo kuelekea mchezo wao wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Manchester UnitedWikiendi hii kufuatia kuumia kwa Harry Kane ambaye anatakiwa kuwa nje kwa maumivu ya nyama za paja.
Spurs imetoa habari hizo asubuhi ya leo wakiwa kwenye maandalizi ya mwisho mwisho kuelekea mchezo huo na United wanaoshika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi.
Wamesema kwamba baada ya kufanyiwa vipimo mapema wiki hii, imegundulika ana maumivu ya nyama za paja la mguu wa kushoto. 
Kane aliumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England Jumapili iliyipita dhidi ya Liverpool. "Kwa kesho, hatuwezi kufanya kosa kumchezesha,"alisema kocha Mauricio Pochettino kuhusu Kane.
"Ni maumivu madogo, madogo sana, lakini hatuwezi kufanya kosa. Tutaona baada ya Jumatano Jumatano dhidi ya Real Madrid. Kesho [Jumamosi] haiwezekani. 
"Ndiyo [ni pigo], wakati wote unataka wachezaji wote wawepo. Ni tatizo. Kucheza zaidi au kucheza kidogo, tunataka wawepo wacheze. Wakati wote tunaamini kwenye umoja, kikosi. Wakati wa msimu, matatizo yanatokea na lazima uwaamini wachezaji wote, kikosi chote,".
Lakini msimu uliopita, ikiwa bila Kane, Spurs ilicheza mechi saba bila kupoteza, tano ikishinda. Kane amefunga mabao 13 katika mechi 12 za Spurs msimu huu.

No comments:

Post a Comment