Waziri Wa Nchi- Ofisi Ya Waziri
Mkuu- (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira Na Watu Wenye Ulemavu Jenista
Mhagama (Mb) akizindua rasmi namba ya kuchangia Mfuko wa UKIMWI ambayo
ina maana katika mwitikio wa UKIMWI Namba hiyo (0684-90, 90, 90); yaani
Asilimia 90 ya watu wanaoishi na VVU wapime afya zao, Asilimia 90 ya
waliopimwa na kukutwa na VVU waanzishiwe dawa na Asilimia 90 ya
walioanza dawa waweze kufubaza virusi.
Waziri wa Nchi- Ofisi ya Rais
TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo(kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa
Manyara Mhe. Joel Bendera hundi ya kiasi cha milioni mia mbili
(200,000,000/=) kwa ajili kusaidia kujenga kituo cha afya Mererani ikiwa
ni ahadi ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kusaidia ujenzi wa
kituo cha Afya katika eneo hilo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera Uratibu Bunge Kazi, Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista
Mhagama amekabidhi hundi ya shilingi milioni mia sita na sitini
(660,000,000/=) kwa Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto kwa ajili ya kununulia Cotrimoxazole Tabs / Suspension za watu wanaoishi na VVU.
Akizungumza wakati akikabidhi
hundi ya fedha hizo leo Jijini Dar es salaam Waziri Mhagama amesema kuwa
dawa hizo ni kwa ajili ya kutibu na kuzuia magojwa nyemelezi kwa wale
wanaoishi na virusi vya Ukimwi.(WAVIU).
Akifafanua Mhagama amesema kuwa
fedha za wafadhili hazijaelekezwa katika gharama ya ununuzi wa dawa hizo
muhimu, hivyo maamuzi ya kununua dawa hizo ni kuziba pengo la gharama
za kudhibiti UKIMWI, kama malengo ya Mfuko wa Udhamini wa Kuthibiti
UKIMWI (ATF) yalivyo.
Pia, Katika hafla hiyo Waziri
Mhagama alikabidhi hundi ya kiasi cha milioni mia mbili (200,000,000/=)
kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara ili kusaidia kujenga kitua cha afya Mererani
kwa ajili kusaidia kujenga kituo cha afya Mererani ikiwa ni ahadi ya
Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kusaidia ujenzi wa kituo cha Afya
katika eneo hilo.
“Licha ya kuwa Kituo hiki
kitasaidia kuboresha afya ya wananchi wote wanaozunguka eneo la
Mererani, lakini pia kijatoa huduma kwa Watu waishio na virusi vya
Ukimwi na kuwa kitovu cha elimu itakayotolewa kwa makundi mbalimbali ya
wananchi katika jitihada za kupunguza maambukizo mapya ya VVU”. Alisema
Waziri Mhagama.
Aidha, Mhe. Mhagama aliongeza
kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na wahisani wa ndani pamoja na
wananchi wenye nia ya kufanya kazi na serikali katika nyanja mbalimbali
ikiwemo udhibiti wa UKIMWI
No comments:
Post a Comment