Tuesday, October 24, 2017

“Nitafunga tu, Salum Machaku



WAKATI wakipambana na kupata nafasi ya kurejea ligi kuu Tanzania Bara baada ya kukosekana kwa misimu isiyopungua 15, jina la kiungo-mshambulizi wa zamani wa Azam FC, Mtibwa Sugar, Simba, Salum Machaku
lilitawala katika vinywa vya wapenzi wa soka Mkoani Iringa na kijana huyu kutoka Morogoro alitoa mchango mkubwa ili kuirudisha VPL timu ya Lipuli FC.
Machaku alifunga jumla ya magoli 13 katika michezo 14 na kuibuka mfungaji bora wa klabu yake na ligi daraja la kwanza msimu uliopita. Kabla ya mchezo ambao timu yake iliifunga Majimaji FC siku ya Jumapili katika uwanja wa Samora, Iringa mambo yameonekana kwenda ‘mrama’ kwa Machaku kwani alikuwa amecheza michezo miwili tu ya Lipuli katika ligi kuu msimu huu.



“Nimefanikiwa kucheza michezo miwili tu hadi sasa katika ligi. Nilimaliza dakika zote 90’ katika mchezo ambao tulitoka suluhu ya Njombe Mji, na ule wa ushindi dhidi ya Stand United ambao sikumaliza dakika 90.” Anasema Machaku nilipofanya naye mahojiano siku ya Ijumaa iliyopita akiwa Iringa.

Kutoka kuwa mfungaji bora wa klabu na ligi daraja la kwanza hadi kuwa mchezaji anayetafuta nafasi ya kucheza hivi sasa ni jambo la kuumiza hasa pale wachezaji wanaopewa nafasi hiyo wanaposhindwa kufunga.

Lipuli FC imefunga magoli manne tu katika michezo 7 ya VPL na Machaku ameanza kuzoea maisha ya benchi katika timu hiyo chini ya makocha Amri Said na msaidizi wake Selemani Matola.
“Ushindani ndiyo humkuza mchezaji. Ukitazama safu yetu ya ushambuliaji utawaona wachezaji kama Busungu, Lambele, Karihe, Wazir, Dotto Kayombo, Moka Shaaban na mimi mwenyewe. Hawa wote wanataka kucheza na kitendo cha sisi kuendelea kushindania nafasi ndiyo kunaifanya timu iimarike.” Anasema mchezaji huyo mshindi mara moja wa VPL.

“Ninajisikia vizuri katika timu hii. Nafasi itakapopatikana nitajitahidi kufanya vizuri kwa manufaa ya timu yangu. Tuna makocha wazuri na wanatusaidia sana. Kumbuka timu yetu ndiyo kwanza imetoka ligi daraja la kwanza hivyo kuna changamoto nyingi ambazo klabu lazima itapitia hasa wakati huu ligi ikiwa mwanzo.

No comments:

Post a Comment