Lazaro
Mambosasa amesema hayo leo alipokuwa akilaani kitendo cha mauaji dhidi
ya polisi huyo wa kikosi cha kutuliza ghasia ambaye aliuwawa na watu
wasiojulikana na kisha mwili wake kutupwa kwenye uzio wa kambi ya FFU
Ukonga.
"Mnamo tarehe 21 majira ya
saa sita za usiku yalitokea mauaji maeneo ya kambi ya polisi Kikosi Cha
Kutuliza Ghasia (FFU) Ukonga Makao Makuu, ilipofika alfajiri mwili wa
askari PC Charles Yanga uliokotwa ukiwa pembeni mwa uzio wa kambi hiyo
ya Ukonga ukiwa umeangushwa chini, huku pikipiki yake ikiendelea kuwasha
taa za 'hazard' mwili ilipochunguzwa majeraha yalionekana kwenye paji
la uso la huyo kijana lakini pia sikio moja lilikuwa limekatwa kabisa na
kuondolewa. Katika ufuatiliaji wa polisi walibaini kuwa polisi huyo
ameuwawa na watu ambao bado tunawafuatilia na hatujafanikiwa kuwatia
mbaroni bado" alisema Mambosasa
Kamanda Mambosasa amesema kuwa watuhumiwa hao wakikamatwa watafikishwa kwenye vyombo vya dola kwa hatua za kisheria
No comments:
Post a Comment